Monday, April 28, 2014

JE ULIKUWA UNAFAHAMU HILI KUHUSU ALI KIBA?..



Licha ya kuwa na kipaji cha mziki ali kiba pia ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu! "he is talented"
Big up Ally k kwa hilo!.. mazoezi kitu cha muhimu!..
By
'The king'

Wednesday, April 23, 2014

PICHA:MWANAFUNZI WA UDSM ALIYEFARIKI KWA AJALI.

R . I . P Neema Mwakajwanga.
Alifariki kwa ajali juzi saa 1 jioni maeneo ya Ubungo. Alikua ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho UDSM , na ni mzaliwa wa mkoani Mbeya.

Tuesday, April 22, 2014

MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI GHAFLA HUKO GABON..








Mchezaji Sylvain Azougoui alifariki uwanjani baada ya kupiga teke ya kichwani
Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke ya kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.
Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya tokeo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelisimamisha kombora lililopigwa langoni mwake, lakini mshambulizi alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.
Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa Bongoville ambalo liko umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.
Source:bbc swahili!









Saturday, April 19, 2014

USHAWAHI ONA HII:WAUMINI NCHINI KENYA KUDEKI LAMI KWA MAJI NA SABUNI.KISA NINI? SOMA HAPA!..


Screen Shot 2014-04-20 at 1.08.01 AM
Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa na Wakenya kuhusu hii ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya kass fm inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la Eldoret Julius lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu’
Source:millard ayo!

Tuesday, April 15, 2014

YANGA WANAJIANDAA KUMALIZA HASIRA ZAO KWA SIMBA.. JE LITAWEZEKANA HILI?...

watani 2

YANGA wanajiandaa kufuta machungu ya kupoteza ubingwa wao msimu huu kwa wana Lambalamba Azam fc kwa kuhakikisha wanaibuka kidedea katika mchezo wa jumamosi (aprili 19) mwaka huu dhidi ya mahasimu wao wa jadi, wekundu wa Msimbazi Simba.
Yanga wapo mjini Moshi, mkoani Kilimanajaro na leo hii wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki na moja ya timu ya mkoani humo.
Charles Boniface Mkwasa `Master`, kocha msaidizi wa Yanga amesema malengo yao ni kuhakikisha wanawafunga Simba hata kama wameshapoteza ubingwa.
Yanga walioambula nafasi ya pili msimu huu na kuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuanoya kombe la shirikisho mwakani wataingia uwanjani kucheza na Simba yenye mwendo wa kusuasua msimu huu.
Hata hivyo nao Simba wamekuwa wakitamba kuwa mechi yao na Yanga watapambana kwa nguvu zote ili kuwaumiza Yanga mara mbili .
Endapo Yanga watafungwa mechi hiyo, basi watakuwa na maumivu ya kupoteza ubingwa na kufungwa na mahasimu wao Simba sc.
Mechi ya Yanga na Simba huvuta hisia za mashabiki wa soka nchini, na hivi sasa kila kona joto limeanza kupanda.
Huwa ni raha sana kwa timu moja kuifunga timu nyingine baina ya klabu hizi kongwe nchini.
Mechi iliyopita ya ligi kuu bara Yanga walishinda mabao 2-1 dhidi ya JKT Oljoro katika dimba la Shk. Amri Abeid jijini Arusha na kufikisha pointi 55 katika nafasi ya pili, wakati Simba walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ashanti ndani ya uwanja wa Taifa na kubakia na pointi zao 37 katika nafasi ya nne.
Wakati timu hizi zikiwa katika maandalizi ya mechi hiyo, taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinaeleza kuwa Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa tarehe 10 Aprili 2014 Makao Makuu ya klabu kilikubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa YANGA SC utafanyika tarehe 15 Juni 2014.
Taarifa za taratibu za Uchaguzi zitatangazwa hapo baadaye na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Mh Alex Mgogolwa.
Hii itakuwa fursa kwa wanachama wa Yanga kuomba nafasi mbalimbali klabuni hapo.
Ikumbukwe kuwa mwenyekiti wa sasa wa Yanga, Yusuf Manji alishawahi kutangaza siku za nyuma kuwa hatagombea tena nafasi hiyo.
Tamko la Manji liliwagusa wana Yanga wengi wenye mapenzi na kiongozi huyo aliyeisaidia Yanga kufika hapo ilipo.
Manji katika muda wake wa udhamini na Uongozi, amekuwa akiifanyia timu mambo makubwa ikiwemo usajili wa wachezaji ghali na kuweza kuweka kambi nje ya nchi hususani barani Ulaya.
Tusubiri kama nia yake ya kutogombea ipo palepale au atabadili maamuzi.
source:shafii dauda blog

OSCAR PISTORIUS AMALIZA KUJITETEA..

Oscar Pistorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp
Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji dhidi ya Oscar Pistorius umemaliza kumhoji mwanariadha huyo.
Oscar aliyekatwa miguu yote miwili anakana kutekeleza mauaji hayo akisisitiza kwamba alidhani marehemu Steenkamp alikuwa jambazi aliyevamia nyumba mwake.
Kabla ya kuanza kusikizwa kesi hiyo, mwendesha mashitaka Gerrie Nel alisema kuwa alitumai kumaliza kumhoji mwanariadha huyo siku ya Jumanne.Anakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka 25 au maisha gerezani, iwapo atapatikana na makosa ya mauaji ya kupangwa.
Alimuomba Jaji Masipa aahirishe kesi wakati wa mapumziko ya pasaka hadi tarehe 5 Mei.

Ameeeleza kwamba mawakili wenzake wanakabiliwa na kesi nyengine 'nzito zaidi' wanazostahili kuzishughulikia pamoja na 'masuala ya kibinafsi'.


Pistorius akitoka mahakamani
Ombi hilo liliungwa mkono na upande wa utetezi, uliosema kwamba kesi hiyo inapaswa kumalizika tarehe 16 Mei kama ilivyopangwa. Jaji alisema atatoa hukumu yake ya ombi hilo siku ya Jumatano.
Siku ya Jumatatu, Bwana Nel alipendekeza kwamba Pistorius anajifanya kuzidiwa na hisia kuficha matatizo anayopata kujibu masuali mazito anayoulizwa.
Jaji Thokozile Masipa alisitisha kwa muda kesi hiyo mara mbili siku ya Jumatatu baada ya Pistorius kuanza kulia.
Muda mfupi kabla kesi kumalizika kwa siku, Nel alisema: " unazidiwa na hisia sasa kwa sababu unaudhika, kutokana na kuwa ushahidi wako huenda si wa kweli."
Mwendesha mashtaka huyo anayejulikana kwa mtindo wake wa kutishia watu anapowahoji, baadaye alimuuliza Pistorius: " Hautumii hisia zako kukwepa kujibu maswali?"

Pistorius alisema akili yake haikumanika kama inavyostahili wakati wa ufyetuaji risasi huo.


Upande wa mashitaka umesema, kuwa Pistorius anatumia machozi yake kama sababy ya kutaka kuhurumiwa
Awali, kwa mara nyengine Nel alimdadisi kwa uzito Pistorius kuhusu wakati alipompiga Bi Steenkamp risasi.
Mwanariadha huyo alisisitiza kwamba hakuna na nia ya kumuua mtu yoyote, alisema: "Nilifyetua risasi kutokana na uoga."
Nel baadaye alisema kwamba Pistorius alibadili ushahidi wake kutoka kusema alikuwa akijikinga na hadi kusema kwamba alifyetua risasi kwa makosa.
Mwendesha mashtaka akasema hii ni kutokana na kuwa ukweli ni : "Ulimfyetulia Reeva risasi."

"Sio kweli," Pistorius akajibu, huku akibubujikwa kwa machozi na kuilazimu mahakama kusitisha vikao kwa muda.

Pistorius alisema yeye na marehemu Steenkamp walibarizi jioni pamoja kabla ashutuke usingizini kutokana na kusikia sauti iliyotoka bafuni.
Mashahidi wa upande wa mashitaka walieleza kusikia mwanamke aliyepiga mayowe, lakini upande wa utetezi unakana ushahidi huo.

source:bbc swahili

king star...

Saturday, April 12, 2014

ISOME HAPA HOTUBA YA TUNDU LISU ILIYO KATISHWA KWA MAKUSUDI NA TBC.....


Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba Mhe. Tundu Lissu alipokuwa akitoa Hotuba ya Maoni ya walio wachache kutoka katika Kamati Na.4 kabla ya Kukatiwa matangazo na Kituo cha matangazo cha TBC

MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

[Kanuni ya 32(4) ya Kanuni za Bunge Maalum, 2014]

UTANGULIZI

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’) ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa suala la muundo wa Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya Sita inahusu ‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya miaka thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya chama hicho imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi.”

Suala hili pia limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka mitatu iliyopita. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba wakati wa kuwasilisha Ripoti ya Tume yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar tarehe 30 Disemba, 2013: “Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu Rasimu ya awali ilipotolewa ... ni Muungano wa Tanzania. Jambo kubwa limekuwa juu ya muundo wa Muungano.”

Umuhimu wa suala hili unathibitishwa pia na uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum kuelekeza kwamba Kamati zake Namba Moja hadi Kumi na Mbili zianze kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Haya ni maoni ya wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne juu ya Sura hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mjadala wa Kamati Namba Nne kuhusu Sura za Kwanza na Sita za Rasimu unathibitisha pia umuhimu wa suala la muundo wa Muungano katika mjadala mzima wa Rasimu. Kama Taarifa ya Kamati yetu inavyoonyesha, Kamati Namba Nne imeshindwa kufanya uamuzi kuhusu suala hili katika ibara za 1 na 60 za Rasimu. Katika ibara ya 1 ya Sura ya Kwanza, wajumbe walio wengi walipata kura 22, ambayo ndiyo theluthi mbili ya kura za wajumbe wote 33 wa Tanzania Bara wa Kamati Namba Nne. Kwa upande wa Zanzibar, wajumbe walio wengi walipata kura 9 ambayo ni pungufu ya kura 13 zinazohitajika ili kufikisha idadi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 19 wa Zanzibar.

Kwa upande wa ibara ya 60, wajumbe walio wengi walipata kura 22 za wajumbe kutoka Tanzania Bara, ambazo ni theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote 33 kutoka Tanzania Bara. Aidha, kwa Zanzibar, wajumbe walio wengi walipata kura 8, ambazo pia ni pungufu ya kura 13 zinazotakiwa kufikisha idadi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 19 kutoka Zanzibar. Kwa sababu hiyo, ibara za 1 na 60 za Rasimu hazikupitishwa au kuamuliwa na Kamati Namba Nne kama inavyotakiwa na kifungu cha 26(2) cha Sheria na kanuni ya 64(1) ya Kanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Sasa tunaomba kwa ridhaa yako, tuwasilishe hoja na sababu za maoni ya wajumbe walio wachache katika Kamati Namba Nne kuhusu Sura hizi mbili ambazo ndio ‘moyo wa Rasimu.’

SURA YA KWANZA

Sura ya Kwanza ya Rasimu inahusu ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Sehemu ya Kwanza ya Sura hiyo inazungumzia ‘jina, mipaka, alama, lugha na tunu za Taifa.’ Ibara ya 1 inaitambulisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; ibara ya 2 inatangaza ‘eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’; na ibara ya 3 inaweka utaratibu wa ‘alama na sikukuu za Taifa.’ Vile vile ibara ya 4 inaweka utaratibu wa lugha ya Taifa na lugha za alama, wakati ibara ya 5 inahusu ‘tunu za Taifa.’

Kwa upande wake, Sehemu ya Pili ya Sura ya Kwanza inaweka masharti ya ‘mamlaka ya wananchi, utii na hifadhi ya Katiba. Ibara ya 6 ya Sehemu hiyo inatoa ufafanuzi wa ‘mamlaka ya wananchi’; ibara ya 7 inafafanua uhusiano kati ya ‘watu na Serikali’; ibara ya 8 inashurutisha ‘ukuu na utii wa Katiba’; na ibara ya 9 na ya mwisho inaweka ‘hifadhi ya utawala wa Katiba.’

IBARA YA 1

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Kama maelezo yake ya pembeni (marginal note) yanavyoonyesha, ibara ya 1 inaitambulisha ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Ibara ya 1(1) inatamka kwamba “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.”

Kwa upande wake, ibara ya 1(2) inafafanua kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.” Mwisho, ibara ya 1(3) inatukumbusha kwamba “Hati ya Makubaliano ya Muungano ... ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne wanapendekeza mabadiliko ya jina la nchi yetu kutoka jina la sasa la ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ kuwa jina jipya la ‘Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.’ Aidha, wajumbe hao wanapendekeza kuacha kutajwa kwa Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 katika ibara ya 1(1) na (3) ya Rasimu. Badala yake, inapendekezwa kwamba Katiba hii ndiyo iwe msingi wa Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.

Kwa mapendekezo haya, ibara ya 1(1) itasomeka kama ifuatavyo: “Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar ni Shirikisho ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.” Kwa mantiki hiyo, ibara ya 1(2) itasomeka: “Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.” Aidha, ibara ya 1(3) itasomeka: “Katiba hii ndio msingi mkuu wa Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.” Zifuatazo ni hoja na sababu za mapendekezo haya.

SHIRIKISHO AU MUUNGANO?

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Katika nusu karne ya uhai wake, nchi yetu imeitwa ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Hata hivyo, katika kipindi chote hicho, Katiba na Sheria za nchi yetu hazijawahi kufafanua kwa uwazi aina au haiba ya ‘Muungano’ huu. Matokeo ya kukosekana kwa ufafanuzi huu ni kwamba katika nusu karne hiyo, kumekuwa na mjadala mkubwa wa kikatiba, kisiasa na kitaaluma kuhusu suala la kama Jamhuri ya Muungano ni dola ya muungano (a unitary state), au ni dola ya shirikisho (a federal state). Majibu ya swali hili yamekuwa na athari za moja kwa utambulisho, haki, maslahi na wajibu wa Washirika wa Muungano huo, yaani Tanganyika na Zanzibar, na hasa kwa wananchi wa nchi hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Kukosekana kwa ufafanuzi wa aina ya muungano wetu haujawa suala la mijadala ya kisiasa na kikatiba peke yake, bali kumekuwa ni chanzo cha migogoro mikubwa ya kisiasa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Migogoro hii ilianza tangu mwanzo kabisa wa Muungano wakati wa sakata la kuwa na ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Magharibi kwa upande wa Tanganyika na ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa upande wa Zanzibar.

Aidha, kati ya mwaka 1964-1967 ulizuka mgogoro mkubwa kuhusiana na uwakilishi wa Zanzibar katika iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania; kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuundwa kwa CCM mwaka 1977, na katika mjadala wa marekebisho ya Katiba wa mwaka na baadae ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar’ mwaka 1983/1984.

Baadae mwaka 1988 ulitokea mgogoro mkubwa uliopelekea kung’olewa madarakani kwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad na baadae kufukuzwa katika CCM; wakati wa harakati za kudai kura ya maoni kuhusiana na Muungano mwaka 1989/1990; wakati wa mjadala wa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1991; wakati wa sakata la Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (Organization of Islamic Countries - OIC) mwaka 1993; wakati wa mjadala wa G-55 na madai ya kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano mwaka 1994, na Uchaguzi Mkuu wa 1995 huko Zanzibar.

Milenia Mpya ilipoanza ilianza na mgogoro kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 uliopelekea mauaji ya Januari 2001 huko Zanzibar. Mgogoro huo ulifuatiwa na mgogoro juu ya suala la ugunduzi wa mafuta visiwani Zanzibar; harakati za kuanzishwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki na hivi karibuni kupitishwa kwa Marekebisho ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 mwaka 2010.

Zaidi ya migogoro hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi zanzibar zimeunda tume na kamati nyingi ili kupata dawa ya ‘Kero za Muungano.’ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar peke yake imeunda tume na kamati 13 katika kipindi kifupi cha miaka 12 kuanzia mwaka 1992 hadi 2004; wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeunda tume na kamati nane kushughulikia matatizo hayo. Licha ya jitihada zote hizo, ‘Kero za Muungano’ hazijapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Tangu miaka ya mwanzo ya Jamhuri ya Muungano kulikuwa na mitazamo miwili tofauti miongoni mwa waasisi na viongozi wakuu wa Jamhuri ya Muungano. Mitazamo hii tofauti inathibitishwa na kauli ya Mwalimu Julius K. Nyerere, mwasisi na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano katika Mkutano Maalum wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika Dodoma kati ya tarehe 24-30 Januari, 1984: “... Muungano wa Tanzania ukiangalia kwa jicho la Zanzibar ni wa shirikisho lakini ukiangalia kutoka upande wa Tanzania Bara ni Serikali moja.”

Mwalimu alikuwa akimjibu Makamu Mwenyekiti wa CCM, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wakati huo, Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi aliyesema kwamba Muungano wa Tanzania umeunda Shirikisho (Federation) na sio Serikali moja (Unitary State). Mjadala huo ulipelekea ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar’ na kung’olewa madarakani kwa Jumbe, Waziri Kiongozi wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Kwaw Swanzy. Aidha, Wolfgang Dourado, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati Hati ya Muungano inasainiwa, na mkosoaji mkubwa wa Muungano huo, aliwekwa kizuizini kwa kuunga mkono hoja za Rais Aboud Jumbe.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Miaka kumi baada ya ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar’ Jamhuri ya Muungano ilikabiliwa na mgogoro mwingine tena wa kikatiba na kisiasa, mara hii ukitokana na Zanzibar kujiunga na OIC. Kitendo hicho kilizua tafrani kubwa ya kisiasa pale Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipopitisha Azimio la kutaka kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano mwezi Agosti, 1993. Azimio hilo liliungwa mkono na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kitendo kilichomfanya Mwalimu Nyerere kuingilia kati na kuzima jaribio hilo.

Baadae Mwalimu aliandika kitabu alichokiita Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania kilichochapishwa mwaka 1994. Katika kitabu chake, Mwalimu anarejea mkanganyiko ambao umekuwepo kuhusu aina ya Muungano huu kwa maneno yafuatayo:

“Nchi zinapoungana na kuwa nchi moja mifumo ya kawaida ya miundo ya Katiba ni miwili: Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafuta serikali yake, na nchi mpya inayozaliwa itakuwa ni nchi moja yenye serikali moja. Katika mfumo wa pili kila nchi itajivua madaraka fulani ambayo yatashikwa na serikali ya shirikisho, na itakuwa na serikali ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyobaki. Mambo yatakayoshikwa na serikali ya shirikisho ni yale ambayo yakibaki katika mamlaka ya nchi zilizoungana, basi kwa kweli nchi hizo zitakuwa hazikuungana kuwa nchi moja, bali zinaendelea kuwa nchi mbili zenye ushirikiano mkubwa katika mambo fulani fulani.... Shirikisho halisi la nchi mbili litakuwa ni nchi moja yenye serikali tatu, Serikali ya shirikisho na serikali mbili za zile nchi mbili za awali zilizoungana kuzaa nchi mpya moja.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mwaka ambao Mwalimu Nyerere alichapisha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Makamu Mwenyekiti wake wa CCM na Makamu Rais wake hadi Januari 1984, Alhaj Aboud Jumbe, aliyekuwa pia Waziri wa Afya wa Zanzibar wakati Muungano unazaliwa na baadae Rais wa Pili wa Zanzibar, naye alichapisha The Partnership: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Miaka 30 ya Dhoruba. Katika kitabu hicho, Alhaj Jumbe anathibitisha kwamba “Ibara za Mkataba wa Muungano ziliweka bayana mfumo ambao serikali kuu na serikali shiriki katika Muungano kuwa na nguvu zinazoendeana, yaani, mfumo wa shirikisho ambao kuna mgawiko wa mahakama, baraza la kutunga sheria na urais baina ya serikali kuu na serikali mbili au zaidi, na kila serikali ikiwa na nguvu kamili ndani ya mamlaka yake.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Aina ya dola iliyotokana na Hati ya Makubaliano ya Muungano haikuwahangaisha waasisi wa Muungano ama viongozi wake wakuu peke yao. Hata ndani ya makorido ya mamlaka, mjadala juu ya suala hili umekuwa mkubwa na umeundiwa Tume na Kamati mbali mbali za kulichunguza. Kwa mfano, hata kabla ya kuchapishwa kwa Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania na The Partner-ship, tarehe 6 Aprili, 1992, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Salmin Amour aliunda Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Kujenga Hoja Juu ya Masuala ya Muungano wa Tanzania, maarufu kama Kamati ya Amina Salum Ali kutokana na jina la Mwenyekiti wake. Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna, ambaye ni mjumbe wa Bunge hili Maalum, alikuwa Katibu wa Kamati hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Kamati ya Amina Salum Ali ililichunguza suala la aina ya Muungano uliozaliwa na Hati ya Makubaliano ya Muungano. Jibu la Kamati hiyo lilikubaliana na nusu ya hoja ya Mwalimu Nyerere na nusu ya hoja ya Alhaj Aboud Jumbe: “... Muungano wa Tanzania, haidhuru unaitwa ‘Union’, lakini uko kati na kati baina ya ‘Union’ na Shirikisho. Kuwepo kwa Serikali ya Muungano yenye madaraka makubwa ni kielelezo cha sura ya ‘Union’. Sura hii inazidi kutiliwa nguvu na kile kitendo cha Tanganyika kuvua madaraka yake yote na kuyaingiza katika Serikali ya Muungano. Kwa upande mwengine kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye madaraka kamili Zanzibar juu ya mambo yote yasiyokuwa ya Muungano, ni kielelezo dhahiri cha sura ya Shirikisho. Kwa hivyo, Muungano huu ni wa aina yake.”

MTAZAMO WA KITAALUMA

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Hati ya Makubaliano ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar imejadiliwa sana na kwa miaka mingi katika ulingo wa kitaaluma. Mjadala huu umehusu, kwa kiasi kikubwa, aina na muundo wa Muungano huu. Katika kitabu chake Tanzania: The Legal Foundations of the Union, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwezi Januari, 1990, Profesa Issa Shivji alisema, baada ya uchambuzi wa kina wa Hati ya Muungano, kwamba Makubaliano ya Muungano yalitengeneza katiba ya shirikisho. Kwa mujibu wa Profesa Shivji, katiba za shirikisho zina sifa kuu zifuatazo ambazo alisema zipo katika Hati ya Muungano:

a. Kuna mgawanyo wa wazi wa madaraka kati ya serikali kuu na serikali za sehemu za muungano ambayo yapo katika ngazi moja;
b. Mamlaka ya serikali kuu yaliyowekewa mipaka ya wazi wakati mamlaka yaliyobaki yako mikononi mwa serikali za sehemu za muungano;
c. Serikali zote, yaani serikali kuu na serikali za sehemu za muungano zinagusa maisha ya wananchi wao moja kwa moja tofauti na serikali ya mkataba (confederation) ambako serikali za sehemu ndizo zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Kwa maneno ya Profesa Shivji, kwa kuyaangalia Makubaliano ya Muungano kutoka upande wa Zanzibar na Tanganyika na kwa ujumla wao, “... msingi wa shirikisho ndio wenye nguvu na Makubaliano ya Muungano yanaweza kutafsiriwa kwa usahihi kama katiba ya shirikisho.” Kwingineko katika kitabu hicho, Profesa Shivji alidai kwamba: “Kwa vyovyote vile, ni wazi kwamba Makubaliano ya Muungano sio katiba ya muungano (unitary constitution).”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Msimamo wa Profesa Shivji kuhusu Makubaliano ya Muungano kuwa ni katiba ya shirikisho umeshikiliwa kwa miaka mingi na wasomi wengine wa Muungano huu. Hivyo, kwa mfano, katika kitabu chao cha Tanzania Treaty Practice kilichochapishwa mwaka 1973, Earl E. Seaton na S.T. Maliti walikubali kwamba Makubaliano ya Muungano yaliunda katiba ya shirikisho na sio katiba ya muungano.

Miaka kumi baadae, Wolfgang Dourado, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati Hati ya Muungano inasainiwa, naye alidai kwamba Makubaliano ya Muungano hayakutengeneza dola la muungano bali yalitengeneza ‘shirikisho la kweli.’ Wasomi wengine ambao wameitaja Katiba ya Tanzania kama katiba ya shirikisho na wala sio ya muungano ni Profesa B.P. Srivastava katika makala yake ya mwaka 1984 ‘The Constitution of the United Republic of Tanzania 1977: Some Salient Features, Some Riddles’, na Profesa Palamagamba J.A.M. Kabudi, katika International Law Examination of the Union of Tanganyika and Zanzibar: A Federal or Unitary State?, ambayo ni matokeo ya utafiti aliouwasilisha mwaka 1986 kwa ajili ya Shahada yake ya Uzamili ya Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 2009 The Legal Foundations of the Union kilichapishwa kwa mara ya pili, mara hii kikiwa na Utangulizi wa Profesa Yash Ghai, Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Kenya iliyozaa Katiba Mpya ya Kenya ya mwaka 2010.

Kwenye Utangulizi wake Profesa Ghai anasema kwamba licha ya Tanzania kutokuwepo katika orodha za mashirikisho zilizoandaliwa na wasomi au na Jukwaa la Kimataifa la Mashirikisho (International Forum of Federations); na licha ya Katiba ya Tanzania kutokutumia neno ‘shirikisho’, bado Tanzania ni shirikisho.

“Tanzania inakidhi vigezo vingi vya rasmi vya shirikisho: mahusiano kati ya sehemu zake tofauti yamewekwa katika katiba, ambayo ni sheria kuu, na hayawezi kubadilishwa katika ushirikisho wao bila kuungwa mkono na idadi mahsusi ya wabunge wa kutoka Zanzibar na Bara ... wakipiga kura tofauti tofauti. Katiba inaweza kufanyiwa marejeo na mahakama. Kuna aina mbili za serikali (serikali kuu na serikali za sehemu za shirikisho), kila moja ikiwa na mamlaka yaliyoainishwa wazi. Kuna mabunge ya shirikisho na ya sehemu yake ... na sheria za shirikisho na za sehemu yake zikitumika katika nchi.”

MTAZAMO WA TUME

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Tume ya Mabadiliko ya Katiba (‘Tume’) imetoa maelezo marefu kuhusu madhumuni, lengo na sababu za mapendekezo ya ibara ya 1 ya Rasimu. Pamoja na mengine, kwa mujibu wa Tume, “... lengo la ibara hii ni kuainisha aina na hadhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni Muungano wa Shirikisho lenye Mamlaka Kamili (Sovereign Federal State). Hatua hii ina lengo la kuimarisha Muungano kwa kuipa Mamlaka ya Kidola Jamhuri ya Muungano na kubainisha utambulisho, uwezo na mamlaka ya Nchi Washirika katika Muungano.”

Malengo mengine ambayo Tume imeyataja malengo mengine kuwa ni “... kuainisha mfumo wa utawala wa Jamhuri ya Muungano na kupanua misingi muhimu ya nchi ...”; na kuonyesha kuwa “Hati ya Muungano ya 1964 ndio chimbuko la Muungano wa Tanzania ... na ... kuipa hadhi ya kikatiba Hati hiyo ... kwa ... (kuiingiza) ndani ya Katiba kama ibara inayosimama yenyewe.”

Tume imetaja sababu za mapendekezo haya kuwa ni kutekeleza matakwa ya kifungu cha 9(2)(a) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, yaliyoitaka Tume “... kuongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano.” Aidha, kwa mujibu wa Tume, mapendekezo haya yatahifadhi asili, taswira na hadhi ya Jamhuri ya Muungano katika jumuiya ya kimataifa kama inavyotakiwa na Mkataba wa Montevideo Kuhusu Haki na Wajibu wa Nchi wa mwaka 1933, ambao unatambua nchi yenye muundo wa shirikisho kuwa ni dola katika sheria za kimataifa.

Tume imetambua ukweli wa kihistoria kwamba kumekuwepo mjadala wa miaka mingi miongoni mwa Watanzania “kuhusu aina ya Muungano uliopo Tanzania iwapo ni shirikisho au la.” Kwa sababu hiyo, pendekezo hili litaondoa “utata wa aina na muundo wa Muungano ambao umesababisha kuvunjwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Serikali zote mbili mara kadhaa.”

Tume iliridhika kwamba Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho. Kwa maneno yake: “Shirikisho hili linatokana na muungano wa hiari wa Tanganyika na Zanzibar ambazo zilikuwa Jamhuri zenye mamlaka kamili kabla ya kuungana tarehe 26 Aprili 1964.” Tume inafafanua kwamba, kwa kawaida nchi ambazo zimeingia katika muungano zinaweza kuchukua moja kati ya sura tatu:

i. Muungano wa Serikali Moja (Unitary State);
ii. Muungano wa Shirikisho (Federation); na
iii. Muungano wa Mkataba (Confederation).
Kwa mujibu wa Tume, “... mfumo wa shirikisho unakuwepo pale ambapo nchi mbili au zaidi zimeungana na hazikuunda serikali moja. Kwa maana hiyo shirikisho ... linamaanisha mfumo wa utawala wa nchi wenye sifa zifuatazo:

1. Kunakuwa na ngazi mbili za serikali zonazotawala eneo moja la nchi na raia wale wale; moja ikisimamia mambo ya muungano (shirikisho) na nyingine mambo yasiyo ya muungano (yasiyo ya shirikisho);
2. Kila ngazi ya serikali, yaani ile ya shirikisho na ile ya nchi washirika inakuwa na mamlaka kamili na maeneo ya utendaji na uhakikisho wa kikatiba wa uhuru wa kutoingiliana baina ya serikali hizo katika maeneo waliyo na madaraka nayo bila ya kushauriana....;
3. Katika muundo huu, serikali ya muungano ndiyo yenye mamlaka juu ya masuala yote yaliyokubaliwa kuwa ya muungano (shirikisho). Serikali za nchi washirika zinakuwa na mamlaka ya kikatiba ya kushughulikia mambo yasiyo ya muungano katika maeneo yao ya utawala; na
4. Katika muungano wa shirikisho mamlaka kuu ya kidola (sovereign powers and functions) yapo chini ya serikali ya shirikisho (muungano).”
Mheshimiwa Mwenyekiti,

Pamoja na kushindwa kufikisha idadi ya kura inayotakiwa na kifungu cha 26(2) cha Sheria na kanuni ya 64(1), Wajumbe walio wengi – karibu wote wanachama wa CCM – wamependekeza kufutwa kwa ibara ya 1(1) na (2) ya Rasimu. Badala yake, wajumbe hao wanapendekeza ibara mpya ya 1(1) isomeke kama ifuatavyo: “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi yenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya Hati ya Makubaliano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.”

Tofauti pekee ya mapendekezo haya na mapendekezo ya ibara ya 1(1) ya Rasimu ni neno ‘Shirikisho.’ Hii ina maana kwamba, licha ya ushahidi mkubwa wa kitaalamu tuliouonyesha hapa, wajumbe walio wengi wa Kamati Namba Nne wanaamini kwamba Jamhuri ya Muungano sio Shirikisho. Kwa mapendekezo haya, wajumbe na wanachama hawa wa CCM wanapendekeza kuendeleza status quo, yaani sintofahamu ya kama Muungano huu ulitengeneza dola ya ki-Shirikisho au dola ya ki-Muungano, ambayo imeugubika Muungano kwa nusu karne ya uhai wake. Mapendekezo haya yataendeleza pia migogoro ya kikatiba na ya kisiasa ambayo imekuwa ni sehemu ya uhai wa Muungano huu katika kipindi hicho hadi kubatizwa jina la ‘Kero za Muungano.’

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Kwa kuzingatia uchambuzi huu, ni wazi kwamba kuendelea kutumia jina la ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ kunaendeleza hisia potofu kwamba Makubaliano ya Muungano yalianzisha dola ya muungano (unitary state) na sio dola ya shirikisho (federal state). Aidha, kufanya hivyo ni kuendeleza migogoro ya kisiasa na ya kikatiba ambayo, kama tulivyoonesha, imetokana na kukosekana kwa ufafanuzi juu ya aina ya muungano uliotokana na Hati ya Makubaliano ya Muungano. Hii, kwa maoni yetu, haiwezi kuwa dawa ya matatizo ya Muungano huu.

Kwa sababu hiyo, ili kuweka wazi aina ya muungano uliozaliwa na Hati ya Makubaliano ya Muungano; ili kuondoa hisia potofu kwamba Makubaliano hayo yalizaa dola ya muungano, ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa ‘Kero za Muungano’, tunapendekeza kwamba maneno ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ yaliyoko katika ibara ya 1 na ya 2 na katika ibara nyingine zote za Rasimu yafutwe, na badala yake maneno ‘Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar’ yaingizwe katika ibara husika.

Mapendekezo yetu yana manufaa makubwa yafuatayo. Kwanza, yanaweka wazi kwamba muungano huu ni wa dola ya ki-Shirikisho na wala sio dola ya ki-Muungano. Pili, mapendekezo haya yanaweka bayana ukweli kwamba ni nchi mbili huru, yaani Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndizo zilizoungana. Uzoefu wa nchi nyingine zilizoungana unaonyesha kwamba jina la muungano huweka bayana kwamba zilizoungana ni nchi zaidi ya moja. Mifano ya wazi ya jambo hili ni majina ya Marekani (United States of America); Uingereza (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland), na Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates). Aidha, Urusi ya zamani ilijulikana kama (Union of Soviet Socialist Republics) na Yugoslavia ya zamani ilikuwa inaitwa Federal Socialist Republics of Yugoslavia.
kingstar
source:mjumbe blog

Friday, April 11, 2014

AZAM WAZIDI KUWANYIMA USINGIZI YANGA. HATARI KWELI...



Na Baraka Mpenja, Dar Es salaam
0712461976
AKIWAANZISHA washambuliaji wake watatu, Gaudence Mwaikimba, Kipre Herman Tchetche na John Rapahel Raphael Bocco 'Adebayor', kocha wa Azam fc Mcameroon, Joseph Marius Omog amefanikiwa kuongeza pointi tatu muhimu baada ya kuwafumua maafande wa Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara, kwenye uwanja wa Mabatini , Mlandizi mkoani Pwani.
Lengo la Omog lilikuwa ni kufunga mabao mengi katika mchezo huo ili kuendelea kujiweka mazingira mazuri ya kuiongoza Azam fc kuandika historia mpya ya kutwaa ubingwa wao wa kwanza tangu wapande ligi kuu mwaka 2008/2009.
Mipango yake ilianza kuzaa matunda dakika ya 8 ya mcheza ambapo mshambuliaji wake ambaye mara nyingi hukalia benchi, Gaudence Mwaikimba kufunga bao la kuongoza.(P.T)
Azam fc walionekana kuwa na uchu wa kupata mabao zaidi, na katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza, winga machachari, Himid Mau Mkami alitia kambani bao la pili kufuatia krosi nzuri iliyochongwa na beki wa kulia, Erasto Edward Nyoni.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa Azam fc kuwa kifua mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilipoanza, Azam fc walionekana kuendelea kuwepo mchezoni ambapo dakika ya kwanza tu, Kipre Herman Tchetche aliandika bao la tatu na kuwanyanyua mashabiki waliofurika uwanjani.
Kwa matokeo hayo Azam fc wamezidi kujikita zaidi kileleni kwa kufikisha pointi 56, pointi nne mbele ya mabingwa watetezi Yanga SC katika nafasi ya pili.
Yanga walikuwa wanaufuatilia mchezo huo kwa makini ili kujiridhisha kama wataweza kutetea ubingwa wao msimu huu.
Jana wanajangwani hawa walishinda mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar na kuwasogelea Azam fc kileleni, lakini leo mambo yamezidi kuwa magumu zaidi kwao kutokana na matokeo ya Mabatini.
Ili kutetea ubingwa wao, Yanga wanahitaji kushinda mechi mbili walizobakiza dhidi ya JKT Oljoro na Simba sc, wakati huo huo wakiiombea mabaya Azam fc ipoteze michezo yote miwili.
Wakati Yanga wakiwa katika presha kubwa, Azam fc wao wanahitaji pointi tatu tu kuwavua ubingwa Yanga.
Wakishinda mechi moja kati ya mbili walizobakiza, wana Lambalamba watafikisha pointi 59 ambazo Yanga hawataweza kufikisha hata kama watashinda mechi zote walizosaliwa nazo kwa mabao 50.
Yanga wakishinda mechi mbili zijazo watafikisha pointi 58 kibindoni ambazo Azam fc wataweza kuzivuka kama watashinda mechi moja tu kati ya mbili walizonazo mkononi.
Mechi ijayo, Azam fc watashuka dimbani dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Hii itakuwa mechi muhimu sana kwa Azam fc, lakini watahitaji kutumia nguvu kubwa kuwafunga wagonga nyundo hawa wa Mbeya kwasababu ya rekodi yao nzuri ya kutofungwa katika uwanja huo.
Mbeya City mpaka sasa wapo nafasi ya tatu katika msimamo wakiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 24.
City wameshapoteza nafasi mbili za juu kwasababu wakishinda mechi mbili zilizobaki watafikisha pointi 52 ambazo zimeshafikiwa na Yanga, huku wakiwa na michezo miwili mkononi.
Hata kama Yanga watapoteza mechi mbili zijazo, kama Mbeya City watahitaji kuwa wa pili watahitaji kushinda mechi mbili zilizobaki kwa ida kubwa mno ya mabao.
Ukiangalia wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, Yanga wametia kambani mabao mengi mno zaidi ya Mbeya City. Hivyo bado nafasi ya pili kwao ni ngumu kuipata.
Hata hivyo kushika nafasi ya tatu si haba kwao kwasababu ni msimu wao wa kwanza.
Wakati Azam fc wakijiandaa kwenda Mbeya, tayari zipo tuhumu kwa wenyeji wao Mbeya City kuwa wamehongwa na wana Lambalamba ili kucheza chini ya kiwango.
Madai ya kuuzwa kwa mechi hiyo yamesambazwa kuhusu mambo matatu;
ambayo ni Timu ya Mbeya City kununuliwa basi na Klabu ya Azam, Kocha wao Juma Mwambusi amejengewa nyumba maeneo ya Chamazi, na wachezaji wao wamepewa fedha ili waweze kucheza chini ya kiwango dhidi ya Azam.
Hata hivyo uongozi wa Mbeya City umekanusha tuhuma hizo na kusema watu wanaosambaza taarifa hizo hawana malengo mazuri na klabu yao, zaidi wanawachafua kwa mashabiki wao.
Bingwa atakayepatikana msimu huu atakuwa ni halali kutokana na ushindani mkubwa uliooneshwa na timu za juu.
Azam fc, Yanga na Mbeya City toka mwanzo wa mzunguko wa pili zimefukuziana mno na hatimaye sasa Mbeya City wamejitoa na kuwaacha Yanga na Azam fc wakiendelea kuchuana.
Sasa Yanga na Azam fc ni kutegeana tu, atakayepoteza mechi atamnufaisha mwenzake.
Lakini Yanga ndio watumwa kwa Azam fc kwasababu wanahitaji kutetea ubingwa wao, wakati huo huo wakihenyeka kutaka kusawazisha pengo la pointi nne dhidi ya Azam fc.
Ligi hiyo itaingia raundi ya 25 Aprili 12 na 13 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani. Aprili 12 mwaka huu itakuwa Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro), Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga), na Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).
Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga), Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Chanzo:www.shaffihdauda.com

Thursday, April 10, 2014

CHEKI JINSI HALI ILIVYOKUWA TETE LEO MWENGE KUHUSU BODABODA KUTORUHUSIWA KUVUKA MWENGE KWENDA POSTA.

 Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa
 Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi.
 Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa
 Huu ni upande wa kutokea Mwenge kuelekea Posta ambapo Bajaji haziruhusiwi kuvuka hapo kuelekea Posta
 Baadhi ya Madereva wa Bajaji na Boda boda wakijadiliana Juu ya swala hilo la kuzuiliwa kuelekea Posta

 Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa

  Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa  kwenda Posta wakitokea Mwenge
 Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa Mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.
Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake  kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.

Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.


"Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo"Hiace" pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa"  alimalizia kwa kusema "Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali" alisema Polisi huyo.

Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo. 

Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.
Picha na Dar es salaam yetu
 

MBEYA CITY WATOA MAELEZO KUHUSU TAARIFA ZA KUHONGWA NA AZAM FC

20140330_160206_095b1.jpg
TAARIFA KWA UMMA
UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu nchini tumezishuhudia .Changamoto hizo ni ikiwemo upangaji wa ratiba usiyokuwa na uwiano mzuri,baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo,wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi,uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda chafu na ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo kama ya Tanzania. Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1.    Klabu imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa ajili ya matumizi mbalimbali  ya Halmashauri ikiwemo kutumiwa na timu zake ( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza  halmashauriilipotangaza  nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender tarehe 8/8/2013o.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01   hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya ndani  kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika gazeti la majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji  wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja ya maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi la wachezaji  taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu. 
Na 
kingstar!

WASTARA: LAZIMA NITAKUFA KWA AJALI TU!...

Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
MASKINI! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amezungumzia jinsi jinamizi la ajali linavyoweza kumsababishia kifo kwani ana msururu mrefu wa matukio hayo, Amani lina mzigo kamili.
Katika mahojiano maalum na gazeti hili yaliyodumu kwa takriban saa mbili kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, Wastara alisema tayari ameshapata ajali kumi tangu kuzaliwa kwake, mbili zikimtokea jirani na nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar.
AJALI YA KWANZA
Wastara ambaye ni mjane wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Kibongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, alisema ajali ya kwanza aliipata mwaka 1987 akiwa na miaka minne.
Alisema ajali hiyo ilimtokea mkoani Morogoro, aligongwa na pikipiki. Mguu wa kulia ulisagika, akakaa miezi kumi nyumbani akiwa hawezi kutembea.
“Nilipopona sawasawa nilianza kutembea kwa kujifunza kama mtoto anavyofanya,” alisema Wastara.
AJALI YA PILI
Nyota huyo alizidi kuweka wazi kwamba, mwaka huohuo alipata ajali ya pili akiwa mkoani humo ambapo aligongwa na baiskeli kisha kuvunjika mkono wa kulia, akafungwa plasta ngumu au hogo (P.O.P).
AJALI YA TATU
Wastara ambaye alitamba na Filamu ya Mboni Yangu alisema mwaka mmoja na nusu baadaye, yaani 1990 alipata ajali ya tatu akiwa na pacha wake aitwaye, Issa Juma.
“Nakumbuka ilikuwa Ramadhan ya kwanza, wakati huo tulikuwa tunaishi Mlandizi (Bagamoyo, Pwani).
“Siku hiyo kuna mzee mmoja alitupa shilingi mia, tukagawana hamsini-hamsini. Mimi nilinunulia maembe. Mwenzangu akakataa kutumia fedha yake, nikamwambia mimi natumia ya kwangu kwa sababu tunaweza kugongwa kabla hatujatumia fedha yetu.
“Kweli haikuchukua muda. Wakati tunavuka barabara pale Mlandizi mbele yetu kuna mtu alikuwa na baiskeli, tukashika nyuma, ile anavuka na sisi tukafuata, ghafla gari aina ya Toyota Coaster lililokuwa likitokea Chalinze kuelekea Dar likatokea na kutugonga mimi na kaka yangu.
“Kwenye ile ajali mimi nilipasuka fuvu (akionesha kovu kichwani), kaka yeye alivunjika mguu wa kushoto,” alisema Wastara na kuongeza:
“Tulipelekwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha. Sikumbuki tulikaa kwa muda gani lakini ulikuwa muda mrefu.”
 
AJALI YA NNE
Kama hiyo haitoshi, staa huyo aliongeza kuwa akiwa na umri wa miaka 15 alianguka kwenye ngazi nyumbani kwao mkoani Morogoro, akavunjika mkono.
 
AJALI YA TANO
“Mwaka 2008, nilipata tena ajali ya pikipiki. Ilikuwa maeneo ya Mwananyamala Sokoni (Dar).
“Dalali niliyekuwa naye alikuwa na pikipiki, nilipanda nyuma akaingia chini ya Toyota Coaster ya Mbagala-Mwenge.
Niliumia magoti na mguu wa kushoto, damu zikatoka. Lakini ajali hii nayo niliishaiona mapema.
“Nasema niliona mapema kwa sababu siku hiyo wakati naondoka nyumbani nilivaa suruali nyeupe lakini nikasema huenda ikachafuka, nikabeba nyingine nyeusi kwenye mkoba jambo ambalo siyo kawaida yangu.
“Baada ya ajali, nilipelekwa hospitali moja maeneo ya Kijitonyama, siikumbuki jina. Nilikuwa nimechafuka kwa matope, ukichanganya na damu ndiyo kabisa ikawa balaa.
“Daktari alipomaliza kunihudumia ndiyo nikakumbuka ni kwa nini niliibeba suruali nyeusi, nikabadili,” alisema staa huyo.
 
AJALI YA SITA
“Hii ndiyo ile kubwa. Ndiyo  iliyonivunja mguu na baadaye ukakatwa. Ilikuwa siku tatu mbele baada ya ajali ya Mwananyamala.
“Siku hiyo nililala kwa Sajuki.Wakati naondoka asubuhi alifika rafiki wa Sajuki anaitwa Hamis. Nilitakiwa kuwahi pale Njia Panda ya Tabata-Bima ili nipande gari kwenda dukani ambako nilikuwa nauza.
 “Sajuki aliazima pikipiki ya Hamis lakini kabla ya kuondoka nilimwambia sitaki anipeleke yeye, maana ataniua, kwa utani na yeye alisema ‘we panda nikakuue’.
“Baada ya mvutano wa kukataa, mwisho nilikubali, lakini nilirudi ndani kwanza na kujiangalia kwenye kioo, nikasema moyoni mbona miguu yangu haijakaa vizuri?
“Kweli, tulipofika Njia Panda, Tabata-Bima kulitokea (Toyota) Corolla, ikasimama kuturuhusu kupita, lakini ghafla nikasikia bung! Halafu nikajikuta nipo mtaroni.
“Nilitaka kuinuka, watu wakawa wanapiga kelele nisisimame nitakufa, nikaendelea kulala. Nilijiuliza hivi kweli nipo salama au?
“Madereva teksi wakanunua mfuko wa rambo, wakautia mguu wangu na kuufunga ili damu ivujie humo na kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili.
“Hali ya mguu ilipozidi kuwa mbaya, nilipelekwa kwa Dk. Baki, Tumbi-Kibaha na baadaye mguu ukakatwa.
 
AJALI YA SABA
“Mwaka 2009 nilikuwa mkoani Njombe eneo la stendi ya mabasi, nikiwa tayari nina mguu wa bandia, mguu huo ulichomoka ghafla. Nilikuwa sijauzoea vizuri. Nilianguka vibaya mno mbele za watu. Niliumia mkono,” alisema Wastara.
 
AJALI YA NANE
“Siku hiyohiyo niliingia chooni kwenye hoteli niliyofikia, cha ajabu nikajipigiza kichwa kwenye sinki, niliumia sana kichwani. Kishindo cha kujipigiza watu wote kwenye hoteli walishtuka na kuja kutaka kujua nini kilitokea,” alisema.
 
AJALI YA TISA
Wastara aliendelea kusimulia: “Baada ya Njombe, nilipata ajali tena maeneo ya Popobawa-Tandale (Dar). Nilikuwa na gari langu dogo, Toyota Vitz. Niliingia chini ya Toyota Coaster, sikuumia ila gari iliumia kidogo. Hapo Sajuki alikuwa ameshafariki dunia.”
 
AJALI YA KUMI
“Hii ndiyo mbichi, ilinitokea Februari 13, mwaka huu palepale Tabata-Bima nilipopotezea mguu wangu. Siku hiyo nilikuwa nakwenda kutoa fedha ATM nikanunue umeme.
“Ile naingia tu barabarani lilitokea lori likanigonga na kunirushia mtaroni na gari langu la Vitz.
“Niliumia tena kichwani, gari lilivunjika vioo na taa,” alisema Wastara jinsi ambavyo msururu wa ajali zilivyokosa kuutoa uhai wake huku akijitabiria kifo cha ajali kwa kusema:
“Yaani ajali ajali kila mara. Nadhani nitakufa kwa ajali. Lakini Mungu ndiyo anajua mimi nitakufaje.” 
MAMA AMWEKEA NADHIRI
Wastara mwenye umri wa miaka 31 sasa ambaye aliolewa ndoa ya kwanza akiwa na miaka 15, alisema akiwa mdogo, mama yake alimwekea nadhiri kwamba kutokana na kuandamwa na jinamizi la ajali akifikisha miaka 15 salama angemfanyia Maulidi jambo ambalo alilifanya.
 
KUNA MKONO WA MTU?
“Ni kweli nahisi kwamba kifo changu kitatokana na ajali lakini siamini kama ni mkono wa mtu. Naamini kila kitu ni mpango wa Mungu. Mimi si mtu wa imani nyingine tofauti na kumtegemea Mungu. Najua ana mipango yake juu ya maisha yangu,” alimaliza Wastara.
Wastara alimpoteza mumewe Sajuki mapema Januari 2, 2013 baada ya kuumwa kwa muda mrefu huku akiachiwa mtoto mmoja.