Sunday, April 6, 2014

Friday, April 4, 2014

TAZAMA VICHWA MBALIMBALI VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA.


DSC 0003 49c78
DSC 0004 63aa9
DSC 0005 aeee1
DSC 0006 e1b39
DSC 0007 3744d
DSC 0008 0c9b7
DSC 0009 4b543
DSC 0010 6feab
DSC 0011 41619
DSC 0012 08371
DSC 0013 1aeee
DSC 0014 d533f
DSC 0015 54143
DSC 0016 22497
DSC 0017 fe934
DSC 0018 2ba38

PICHA YA RAISI OBAMA YAZUA KIZAAZAA.


Ortiz amekana madai ya kulipwa na kampuni ya Samsung kwa picha hiyo
Ikulu ya Whitehouse imeikashifu kampuni ya simu ya Samsung kwa kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyojipiga na mchezaji maarufu nchini Marekani David Ortiz kama tangazo la kibiashara.

Hata hivyo kampuni ya Samsung iliisambaza kupitia kwa mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki.
Msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara.
Wakuu wa Samsung hawajasema lolote kuhusu malalamiko ya White House.
Bwana Carney amesema kuwa mawakili wa White House wanashauriwa kuhusu kitendo hicho cha Samsung.
"bila ya kusema mambo mengi, nataka niwaambie tu kwamba White House inapinga vikali jambo hili,'' alisema Carney
Ortiz alimpa Rais Obama Jezzi maalum kutoka kwa klabu anayochezea ya Red Sox ikiwa na jina la Rais siku ya Jumanne na jkisha kumshawishi kujipiga naye picha mwenyewe inayojulikana kama 'Selfie'.
"Nilimpa Jezzi na wapiga picha waka wanatupiga picha, basi nilijhisi na mimi kujipiga naye picha'' alisema mchezaji huyo.

Alikana kuwa kampuni ya Samsung ilimlipa pesa kwa picha hio.

Wednesday, April 2, 2014

SPIKA WA BUNGE LA A.MASHARIKI MASHAKANI KUONDOLEWA.

Chanzo ni nini? hebu soma mwenyewe hapa......


Vikao =vya bunge la Afrika Mashariki
Mgogoro wa uongozi umezuka katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo wabunge wa bunge hilo wanakusudia kumwondoa madarakani spika wa bunge hilo.
Tayari wabunge hao wameshakusanya saini 36 kutoka kwa wabunge 45 wa bunge hilo ambazo zinatakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Wabunge hao wanamlaumu Spika huyo kwa kukiuka kanuni za bunge pamoja kushindwa kuwashirikisha wabunge kwenye baadhi ya uamuzi.
Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa wabunge hao kwa niaba ya wabunge wenzake wa bunge hilo Abudulla Ali Hassani Mwinyi, amesema wabunge hao wamefikia hatua hiyo ya kumwondoa spika huyo Margareth Zziwa kufuatia kukerwa na mwenendo wake.
Tayari wabunge hao wameshapeleka hoja ya kumwondoa spika huyo kwa Katibu wa Bunge hilo ikiwa na sahihi za wabunge 36 ili kutimiza matakwa ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo ili kuanzisha hoja ya kumwondoa spika.
Je wabunge hao hawakuwa na njia nyingine kumaliza mgogoro huo hadi kufikia hatua ya kutaka kumwondoa spika huyo.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo umesababisha kuahirishwa kwa bunge hilo tangu jana kwa muda usiojulikana baada ya spika huyo kuamua kuliahirisha kwa muda usiojulikana.
Hii inafuatia malumbano yalijitokeza ndani bunge hilo ambapo mmoja wabunge alisema hoja hiyo isingeweza kujadiliwa.
BBC ilifanya juhudi za kuwasiliana na spika huyo Margareth Zziwa kwa simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo hata hivyo alikataa kusema chochote ambapo alishauri apigiwe afisa habari wa bunge hilo ili atoe ufafanuzi.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo bado haijajulikana utamalizika lini lakini kwa vyovyote vile utakuwa umeathiri shughuli za Bunge hilo la Afrika Mashariki.

WAATHIRIWA WA MABOMU YA OSAMA TANZANIA KULIPWA FIDIA

Shambulizi la kigaidi lililotikisa Tanzania mwaka 1998
Watanzania walioathirika na mlipuko wa mabomu katika ubalozi wa Marekani yaliyopangwa na Osama bin Laden mjini Dar es Salaam wameshinda kesi yao na sasa watalipwa fidia.
Katika hukumu iliyotolewa na Jaji wa mahakama kuu ya Marekani Thomas Bates mjini Columbas, familia tisa za watu waliokufa na waliojeruhiwa watalipwa jumla ya dola laki nne na ishirini za Marekani.
Hukumu hii inakuja kufuatia kesi iliyofunguliwa mwaka 2000 kwa msaada wa wanasheria wa kimarekani.Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo huyo alitoa hukumu ya awali tangu mwaka 2011 na kilichokuwa kimebaki ni utoaji wa fidia hiyo.
Mmoja wa waathirika hao Judith Mwila ambaye mume wake alifariki katika mkasa huo, amezungumza na mwandishi wa BBC Baruan Muhuza mjini Dar es salaam na kusema kuwa yeye amepata taarifa hiyo kupitia kwenye gazeti tu.
Msimamizi wa waathirika hawa Fuad Latif ambaye ni kiungo kati yao na mawakili wanaoendesha kesi hiyo, ameiambia BBC kuwa Mahakama hiyo inaandaa utaratibu wa kukamata baadhi ya mali za serikali ya Iran na Sudan kwa ajili ya kulipia fidia hiyo.
Nchi hizo zinadaiwa kuhusika na mipango ya kukamilisha milipuko hiyo kwa kumsaidia Osama bin Laden kutekeleza ukatili huo kwa kutumia kundi lake la Al Qaida.
Watu kumi walikufa katika kadhia hiyo ya ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam mwaka 1998.

Kijana Mtanzania Ahmed Ghailani anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani baada ya kukutwa na hatia ya kupanga mashambulizi katika balozi za Marekani mjini Nairobi na Dar es Salaam.
source:bbc news

KISA CHA HAYA YOTE NI MATATIZO YA NDOA YAKE. KIUKWELI INASHANGAZA SANA!.



Matumaini aliyosalia nayo mwanamume huyo ni ya kwenda mbinguni
Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift Valley

Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.Mwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.

RAIS JACOB ZUMA KUJIELEZA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI KUHUSU NYUMBA YAKE.

Nyumba hii iligharimu dola milioni 23 kwa ukarabati
Rais Jacob Zuma anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya Bunge la A-Kusini kujieleza kuhusu kashfa ya kufuja pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya kifahari.
Ukarabati huo uligharimu dola million 23 na Bw Zuma ameamrishwa na mkaguzi au mlinzi wa mali ya umma nchini humo alipe baadhi ya pesa hizo .
Zuma alisema Jumatatu kuwa sio sawa kwake kutakiwa alipe sehemu ya pesa zilizotumiwa kwa ukarabati wa nyumba yake kwani sio yeye aliayeamuru ukarabati huo.
Alisema kuwa maafisa wa serikali ndio walioagiza ukarabati huo bila ya kumshauri.

Zuma alizungumza kwa mara ya kwanza Jumatatu tangu kashfa hiyo kujulikana akisema kuwa halipi chochote kwani hakuomba ukarabatai kufanywa.
source:bbc swahili