Wednesday, April 9, 2014
MAAJABU:CHEKI JINSI HARUSI HII ILIVYOFUNGWA HUKU WAHUSIKA WAKIWA UCHI...NI BALAA TU!.
Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni,hapa bongoland na sehemu nyingi duniani kwa ujumla maharusi mara nyingihujipangia mavazi yao kwa ajili ya siku ya harusi yao huku wakitumia gharama
nyingi kununulia nguo hizo kama mashela ya gharama na suti za maana na kali.Lakini huko New zealand hayo yote hayaitajiki kwan maharusi hufunga ndoa wakiwa watupu kabisa!!Hawa wanajiita Lowes’ Unclad wedding wakidai wanaonesha uhalisia katika nyanja hiyo.
Na wasimamizi wao nao mtindo ule ule!
kweli dunia it's about to end maana hivi sio vya kawaida hata kidogo...
Tuesday, April 8, 2014
OSCAR PISTORIUS AANZA KUJITETEA NA KUJUTA MAHAKAMANI..
Oscar Pistorius akilia alipokuwa chumba cha mahakama Februari 2013
Oscar Pistorius akiwa amejaa majonzi ameanza kujitetea katika kesi ya mauaji inayomkabili kwa kuiomba radhi familia ya Reeva Steenkamp.
Kwa sauti ya kutetema, amesema alikuwa "akijaribu kumlinda" na amesema anashindwa kujua uchungu wanaoupata.
Waendesha mashitaka wanasema Pistorius alimuua Steenkamp mwezi Februari 2013 baada ya kuzozana. Pistorius anasema alidhani ni jambazi.Bwana Pistorius amesema anasumbuliwa na"ndoto za kutisha" na mara nyingi aliamka na kusikia harufu ya damu ya Bi Steenkamp.
Mwanaridha huyo mwenye ulemavu wa miguu amewaambia ndugu wa Bi Steenkamp kwamba "hakuna wakati ambao ameshindwa kufikiria juu yao tangu mkasa huu utokee".
"Naamka kila siku asubuhi na ninyi ni watu wa kwanza kuwafikiria, watu wa kwanza ninaowaombea. Sifahamu uchungu na mawazo na ukiwa ambao nimewasababishia ninyi na familia yenu.
" Nilikuwa najaribu kumlinda Reeva. Nawahakikishia kuwa alipokwenda kulala usiku ule alihisi kupendwa".
"nimejaribu kuandika maneno yangu mengi kwenye karatasi. Mara nyingi kuwaandikia. Lakini hakuna maneno yatakayotosheleza maelezo yangu."
Amesema anatumia dawa za kuzuia msongo wa akili na kukosa usingizi.
"Naogopa kulala, Nimekuwa na ndoto za kutisha, Nasikia harufu ya damu na kuamka nikiwa mwoga.," amesema.
Amesema kamwe hataki kumiliki silaha
Source:bbc swahili
MIAKA MIWILI BAADA YA KIFO CHA KANUMBA:SOMA MANENO ALIYOYAANDIKA LULU KUHUSU KANUMBA..
Leo ni siku ya kutimiza miaka miwili tangu kutokea kwa kifo cha Steven Kanumba aliyekuwa starmkubwa wa filamu na kufanikiwa kutoa njia kwa tasnia ya filamu nchini. Kupitia mtandao wa kijamii Elizabeth Michael "Lulu" ambaye anakabiriwa na kesi ya mauaji ya Kanumba bila kukusudia ameandika kwa uchungu kuonyesha kuwa mpaka leo bado haamini kuwa Kanumba alikwishafariki.
Kupitia mtandao mmoja maaruffu wa kijamii,
Lulu ameandika
"bado Siamini kama mwaka wa pili unakatika bila kukuona wala kukusikia baba, Ninaamini bado tupo nawe kiroho na ninaamini zaidi nasfi yako huko ilipo inasimama kunitetea na kunipigania. Inaweza kuchukua miaka na miaka kukuelezea. You still live in me daddy and you are dearly missed. R.I.P daddy yangu".
Monday, April 7, 2014
Sunday, April 6, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)
