Saturday, May 2, 2015

ALI KIBA AVAMIWA NYUMBANI KWAKE JIJINI DAR.


IMG-20150502-WA0007
     

IMG-20150502-WA0002


IMG-20150502-WA0000


IMG-20150502-WA0001


IMG-20150502-WA0003

Usiku wa kuamkia leo msanii Ali Kiba akiwa nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar-es-salaam, amevamiwa na kundi la watu wapatao 15 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Watu hao waliokuwa na silaha za aina tofauti yakiwemo mapanga,visu na silaha za moto walifanikiwa kuvunja milango na kuingia ndani kisha kuwadhuru baadhi ya ndugu wa ali kiba na kuiba mali pamoja na kila kitu walichoweza kubeba.
   Baada ya abdu kiba kuhojiwa alisema kwamba yeye alikuwa masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao. Waliovamia waliruka ukuta saa tisa za usiku, wakavunja mlango wa sebuleni, wakawakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, waliwapiga na kuwalazimisha waoneshe chumba ambacho Ali kiba yupo. Wale vijana wakajibu kwamba ali hayupo wakauliza chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu kiba. 
    Wameingia chumbani wakamkosa Ali kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia pamoja na pesa milion 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu kiba.
Abdu kiba akatoa taarifa polisi, wakafika usiku huo huo na kuanza ukaguzi eneo lote la nyumba,
Da! inasikitisha sana kwa taarifa hizi!..

Sunday, April 26, 2015

MO MUSIC - NITAZOEA NEW MP3 DOWNLOAD.


                                               
                                                        Mo music-Nitazoea mp3

                                          Download

Sunday, April 12, 2015

HII NDIO HALI HALISI YA VITAMBULISHO VYA UTAIFA MOROGORO





Na hivi ndivyo mambo yanavyoendelea mkoani Morogoro ambapo wanafunzi wa chuo kikuu cha SUA Morogoro wapo katika harakati za kufuatilia vitambulisho vya utaifa kutoka NIDA. Katika suala hili kumekuwa na changamoto mbalimbali kama vile kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu namna ya kujaza fomu kwa usahihi na mambo mengine kama kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu mpaka mtu uje upate kitambulisho hicho.
Baada ya kuzungumza na mmoja kati ya watu wa NIDA kuhusu changamoto ya kuwaelimisha watu kuhusu namna ya kujaza fomu hizo, Mheshimiwa huyo alisema kwamba watu inatakiwa wawaulize wengine wamejaza vipi hizo fomu au wanaweza kuitumia fomu ya mfano iliyobandikwa ili kufatisha namna ya kujaza vema hizo fomu.
Idadi ya wanafunzi ambao washafanikisha suala hilo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi
waliopo chuoni hapo.Kwa sasa mambo yanaendelea vizuri na muda wa kufuatilia vitambulisho hivyo umeongezwa ili huduma hii iweze kutolewa kwa wote kama inavyotakiwa.

Sunday, March 8, 2015

JE UNALIFAHAMU HILI KUHUSU MZEE KIZITO WA SIRI YA MTUNGI?


Jina lake kamili anaitwa Nkwabi Ng'hangasamala. Ni msanii/muigizaji maarufu anayeng'ara sana katika  tamthilia ya SIRI YA MTUNGI. Watu wengi hawafahamu kwamba uyu mzee ni Professor wa chuo cha sanaa Bagamoyo. Ni mzee ambaye anajua kuuvaa uhusika pale anapokuwa anaigiza kiasi kwamba ameweza kuwavutia watu wengi kuifuatilia tamthilia hii ya siri ya mtungi ambayo hivi sasa ndio imefikia tamati.