Thursday, March 20, 2014

BAO LA KAVUMBAGU DHIDI YA AZAM LAMUUA SHABIKI WA YANGA.


SHABIKI wa Timu ya Yanga SC, Deodatus Isaya Lusinde, mkazi wa Kipunguni A, amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla wakati akishangilia bao la Yanga lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza.
Marehemu amepoteza maisha akiwa chumba cha matibabu mara baada ya kuwekewa mashine ya oksijeni na taarifa kuhusu kifo cha shabiki huyo zimethibitishwa na mmoja wa madaktari aliyemhudumia akiwa uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor Matuzya.
Bwana Isaya alikuwa Meneja wa Bar ya Rose Hill iliyopo Segerea jijini Dar. Ameacha mke aitwaye, Rose William Lusinde ambaye ni askari magereza.
Marehemu amekutwa na mauti hayo wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya timu yake ya Yanga na Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mungu ailaze roho ya mwanamichezo, Deodatus Isaya Lusinde mahali pema peponi. AMEN!

Wednesday, March 19, 2014

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA KAMPENI YAANZA VIZURI CHALINZE.

Maandalizi ya mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge kupitia CCM jimbo la Chalinze yaendelea vizuri ambapo jioni ya leo Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajiwa kuhutubia wakazi wa Chalinze na Vitongoji vyake pamoja na kumnadi mgombea wa ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.

 Barabara Kuu iendayo mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha ikiwa imependeza kwa bendera za CCM ,ambapo masaa machache yajayo kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za ubunge CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mratibu wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze akisoma vichwa vya habari vya magazeti ya leo kwenye moja ya vibanda vya magazeti Chalinze huku sehemu kubwa ya maeneo yote yakiwa yamebandikwa mabango yenye picha za mgombea kiti cha ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
 Mratibu wa Kampeni za Ubunge CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye akibadilisha na Kamanda wa Vijana mkoa wa pwani wakati wa kukagua hatua za mwisho za maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa Kampeni.
 Shumina Sharif Kiongozi wa kampeni kata ya Msata na Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa akiwa na mratibu wa kampeni za ubunge za CCM jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni jimbo la Chalinze.
Mratibu wa Kmapeni za Chalinze CCM Nape Nnauye akijadiliana jambo na maofisa wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM jimbo la Chalinze.


Na
'The king'



Saturday, March 8, 2014

KWANI UYU JAMAA ANAOGOPA NINI?

DIAMOND: NAJUTA KUWA STAR




Exclusive Interview! Staa anayeuza zaidi kwa sasa kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefungukia skendo ambazo zimekuwa zikimtafuna kila kukicha huku akieleza kuwa, sasa anajuta kuwa staa, Ijumaa lina mzigo kamili.

Akizungumza na paparazzi wetu katika mahojiano maalum wiki hii, Diamond alisema kuwa amekuwa akivumilia mengi ambayo yanaelekezwa kwake lakini sasa imefika wakati yanamuumiza kwani naye ni binadamu, ana moyo wa nyama na siyo chuma.

Ni kweli unatumia ndumba kutafuta mafanikio?
Diamond: “Baadhi ya watu wanakuwa na imani hizo kuwa mimi natumia mambo ya kishirikina kutafuta mafanikio lakini kwa wasiojua ni kwamba kila nifanyalo namtegemea Mungu na muongozo wa mama yangu mzazi (Sanura Kassim a.k.a Sandra).

“Hao ukijumlisha na jitihada zangu mwenyewe na kujituma sana ndiyo wanaonifanya niwe hapa nilipo leo.

“Si kwa sababu ya mambo ya kishirikina. Kwanza siamini katika ushirikina.”

Hili la mama Wema Sepetu kudai umemloga Wema likoje?
“Sijawahi kumsikia mama Wema akisema nimemloga Wema na hata kwenye magazeti sijaona ila siku nikimsikia ndiyo naweza kusema chochote juu ya hilo.”

Unazungumziaje madai ya wizi wa nyimbo za wasanii wenzako?
Diamond: “Kwa hatua niliyofikia mimi si mtu wa kuiba wimbo wa mtu, bali wapo baadhi ya watu wanaopenda kunisukumia skendo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

“Wakati mwingine wanaotuponza ni maprodyuza ambao huenda siku za nyuma walitengeneza biti kali kwa ajili ya msanii fulani, msanii huyo akaingia mitini.

“Siku unakwenda studio kwake anakusikilizisha biti hiyo na ukiiona kali anakuambia uilipie utengeneze ngoma.
“Baadaye ndiyo unasikia msanii mwingine anaibuka na kusema kaibiwa biti au wimbo. Sasa hapo kosa ni la nani?

Kwa nini una msururu wa mademu?
Diamond: “Mimi ni Sukari ya Warembo na ni kweli baadhi nilikuwa nao kwenye uhusiano lakini wengine ni maneno ya watu tu, sijawahi kutoka nao.

“Kuna ambao wanajitafutia umaarufu kupitia kwangu kwa kusema nimetembea nao lakini siyo kweli. Si unajua ukizungukwa na uaridi na wewe unanukia uaridi? Ndivyo hivyo, wapo baadhi wanajitangazia tu ili wapate umaarufu.”

Baadhi ya warembo ambao tayari ameshaelezwa kutoka nao kimapenzi ni pamoja na Rehema Fabian, Pendo Maisha Plus, Jacqueline Wolper, Natasha, Najma Shaa, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.

Unazungumziaje U-freemason wako?
Diamond: “Mimi siamini juu ya imani hiyo kabisa na sijui kama ipo. Huenda mavazi wakati mwingine yanafanya watu wanahisi hivyo. Kama ni mafanikio niliyonayo, yanatokana na kazi zangu za muziki ambazo kila mmoja anaona.

“Naweza kusema napata shoo nyingi ambazo nalipwa pesa nyingi na mimi situmii pesa yangu kwa anasa. Nawekeza ili baadaye mali zinisaidie nitakaposhuka kimuziki. Huwezi kuwa juu muda wote hivyo ni lazima niwe na tahadhari.”

Ni kweli unawapa mademu mimba kisha kuwatosa hivyo wanachoropoa?
Diamond: “Mabinti wanaoibuka na kusema nimewapa mimba ni walewale wanaotafuta umaarufu ‘kick’ kupitia mimi. Ndiyo maana kuna yule aliyeibuka na kuandikwa na magazeti lakini baadaye alikanusha mwenyewe.

“Najiheshimu na namjua Mola, najua kufanya hivyo ni sawa na kuua.”
Kwa mujibu wa Diamond, kumekuwa na baadhi ya wasanii wenzake ambao wamekuwa wakimchonganisha na mastaa wenzake, mfano ukiwa ni hivi karibuni ambapo alizushiwa kumkandia Ali Kiba ili waingie kwenye bifu.

HII STYLE YA KUSOMA NI BALAA! MCHEKI HUYU!

Wednesday, March 5, 2014

MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MJI WA MAKAMBAKO ZALETA SHIDA NDANI YA MJI

Hivi karibuni kumekuwa na mvua kubwa  ndani ya mji wa makambako zinazosababisha watu kushindwa kufanya shughuli zao vizuri kutokana na mvua kuwa kubwa mno. Wafanyabiashara na watu wengine pia wamekuwa wanaathirika sana na tatizo hili kwani wanashindwa kufanya biashara pindi mvua hizo kubwa zinaponyesha!