Monday, February 24, 2014

VICHWA VYA MAGAZETI MBALIMBALI YA LEO TAR 24 FEB

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

TIMBULO NA PENZI LA SKAINA..

TIMBULO NA PENZI LA SKAINA

Stori: Mayasa Mariwata
CHIPUKIZI wa Bongo Fleva, Ally Timbulo amefunguka kuwa alimwagana na mwigizaji Skyner Ally ‘Skaina’ kwani aligundua kuwa ana uhusiano na Mbongo Fleva mwenzake, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Skyner Ally ‘Skaina’.
‘Akikonfesi’ mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda, Timbulo alisema ishu hiyo ilitokea miaka kadhaa iliyopita ambapo ‘alimsarendia’ mlimbwende huyo ili awe mpenzi wake na aliposhtuka kuwa ana uhusiano na Nay wa Mitego, fasta alibadili uelekeo.
Ally Timbulo.
“Daah! Nilipogundua ana uhusiano na Nay, fasta nilimpotezea,” alisema Timbulo, alipotafutwa Skaina, alisema: “Usiniulize hizo habari, ulivyosikia ndiyo hivyohivyo.”

OKWI ARUHUSIWA NA CAF KUIVAA AL AHLY.

Caf wamruhusu Okwi kuivaa Al Ahly

Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi.
Hans Mloli na Khadija Mngwai
SHIRIKISHO la Soka Afrika (Caf), limemhalalisha mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi kuitumikia klabu yake hiyo rasmi kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuituma leseni yake nchini.
Awali, leseni ya mchezaji huyo raia wa Uganda, ilizuiwa na shirikisho hilo lenye makao yake makuu nchini Misri kutokana na utata wa awali juu ya usajili wa mchezaji huyo.
Caf ilituma leseni za wachezaji 25 watakaoitumikia klabu hiyo kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa huku jina la Okwi likisalia wakisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya TFF kuomba kujiridhisha juu ya usajili wa mchezaji huyo akitokea SC Villa ya Uganda.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, tayari leseni ya Okwi imeshatumwa na sasa yupo huru kuichezea Yanga kwenye michuano hiyo ya kimataifa.
“Leseni ya Okwi imeshatumwa, yupo tayari sasa kuichezea Yanga kwenye mashindano ya kimataifa, nafikiri leo (jana) baadaye au kesho (leo) tutawatumia taarifa rasmi Yanga kuhusiana na suala hili,” alisema Mwesigwa.
Kukwama kwa leseni hiyo, kulisababisha Okwi kukosa michezo miwili ya awali ya michuano hiyo dhidi ya Komorozine ya Comoro ambapo sasa ataanza kuitumikia Yanga kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar, Machi Mosi, mwaka huu.  
Kwa upande wake Okwi aliyecheza mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na Yanga juzi Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting na kuonyesha uwezo mzuri, amesema amejiandaa vyema dhidi ya Aly Ahly ya Misri.
Yanga inatarajia kukutana na Al Ahly Machi Mosi, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa jijini Dar.
Yanga ilifanikiwa kuingia hatua ya pili baada ya kuiondoa Komorozine ya Comoro kwa idadi ya mabao 12-2 nyumbani na ugenini.
“Namshukuru Mungu kuweza kufanikiwa kucheza na tumejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo unaofuata, naamini tutafanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu.
“Tunajua Al Ahly ni timu nzuri na ni ya kiushindani, hivyo tunahitaji kujipanga ili tuweze kufanikiwa kufanya vizuri katika mchezo huo na mechi nyingine za ligi.
“Siwezi kuzungumza kuhusu Simba kunizuia kutocheza kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Yanga hivi sasa na ninataka kuitumikia Yanga na siwezi kuizungumzia timu ambayo sipo kwa sasa,” alisema Okwi.

TAMBWE HAKAMATIKI.

              'na mwandishi wetu "the king star"
Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe.
Na Phillip Nkini
ZIKIWA zimebaki mechi saba ili Ligi Kuu ya Tanzania Bara imalizike, mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe, ameshafikisha idadi ya mabao yaliyofungwa na Kipre Tchetche, msimu uliopita.
Kipre, msimu uliopita alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 17 kwenye ligi kuu, lakini mabao mawili ambayo Tambwe alifunga jana yameshamfanya afikie idadi hiyo.
Hii ni rekodi mpya inawekwa na mshambuliaji huyo raia wa Burundi ya kufikia idadi ya mfungaji bora wa msimu uliopita zikiwa zimebaki mechi nyingi.
Kipre msimu huu hayupo kwenye kiwango kizuri hali ambayo imekuwa ikimpa nafasi kubwa Tambwe ya kuwika kwenye mbio za ufungaji bora.
Nyuma ya Tambwe ambaye huu ndiyo msimu wake wa kwanza, yupo Kipre mwenye mabao 10 na Elias Maguli tisa, hali ambayo inaonyesha ni vigumu kumkuta kinara huyo.
Tambwe anashikilia rekodi nyingine ya kufunga mabao matatu hat trick mbili kwenye michezo miwili ya ligi hiyo msimu huu na inaonekana kuwa anaweza kufunga mabao mengi zaidi na kuweka rekodi nyingine kuanzia ligi imeanza kuchezwa na timu 14.

Sunday, February 23, 2014

TANGAZO LA MUHIMU KWA WALE WALIOOMBA NAFASI ZA KAZI SERIKALINI.

Serikali inapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi kwa tangazo la tarehe 27 Novemba, 2013 wa kada za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Udereva kuwa usaili utaanza tarehe 4 Machi, 2014 takriban katika mikoa yote Tanzania Bara na kituo cha Zanzibar. 
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea kwa lengo la kufahamu masuala mbalimbali ya uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini. Amesema usaili huo unaoanza tarehe 4 Machi katika mikoa takribani yote nchini utahusisha jumla ya wasailiwa6,075 wa fani za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na udereva.  Amefafanua kuwa vigezo vya kupanga mikoa ya usaili kwa wasailiwa wa kada zisizo za maafisa vimetokana na anwani ambazo waombaji waliwasilisha katika barua zao za maombi husika ya kazi.
Daudi alibainisha kuwa kila mwombaji aliyekidhi vigezo na kuchaguliwa kwa ajili ya usaili anapaswa kwenda kufanyia usaili katika mkoa aliopangiwa kama anwani yake inavyoonyesha katika tangazo kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, isipokuwa kwa waombaji wa mkoa wa Katavi wao wataenda kufanyia usaili mkoa wa Rukwa na waombaji waliotumia anwani za mkoa wa Singida wao watafanyia usaili mkoa wa Manyara kutokana na sababu zisizozuilika. 
Aliongeza kuwa kwa mwombaji ambae hatazingatia anwani, siku na muda aliopangiwa na kuamua kwenda mkoa mwingine tofauti na utaratibu uliopangwa ajue wazi hatasailiwa kwa kuwa ratiba na idadi ya majopo ilishapangwa kwa kila mkoa na haitabadilishwa ili kuweza kurahisisha kazi hiyo kukamilika  kwa ufanisi.
Aidha, amewataka waombaji wote wa tangazo hilo kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz  wao wenyewe ili kuweza kujua kiundani endapo wamechaguliwa kufanya usaili, kufahamu tarehe, mahali na muda wa kuanza usaili ili kuepuka usumbufu usiokuwa na lazima. 
Daudi aliendelea kufafanua kuwa kwa waombaji waliotumia anuani za mkoa wa Dar es Salaam kwa nafasi ambazo sio za maofisa usaili utafanyika tarehe 11 Machi, 2014. Aidha, kwa nafasi za Maofisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wote usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 14 Machi, 2014. 
Katibu  amewataka waombaji wote kuhakikisha pindi wanapoenda kwenye usaili wawe wamejiandaa vya kutosha ikiwemo kubeba nyaraka muhimu hususani vyeti halisi vya taaluma zao maana vitahitajika kwa ajili ya uhakiki siku ya usaili. Aidha, amewasihi waombaji wa matangazo mengine ya nafasi za kazi kuwa na subira wakati uchambuzi ukiendelea na pindi utakapokamilika wahusika watataarifiwa.
Alimaliza kwa kuwasisitiza wadau wa Sekretarieti ya Ajira kuwa pindi wanapoona matangazo ya kazi, ikiwemo kuitwa kwenye usaili au kupangiwa vituo vya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari hususani baadhi ya mitandao ya kijamii wajiridhishe kwanza kwa kuangalia taarifa hizo katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, ili kuepuka taarifa zisizokuwa za kweli ambazo zimekuwa zikitolewa nyakati nyingine na baadhi ya watu wasio waaminifu kwa lengo la kupotosha Umma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa   Umma. 21 Machi, 2014 
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz, facebook page www.facebook.com/sekretarietiajira au simu 255-687624975.

Kwa maelezo ya kina na uhakika zaidi kama bado ulikuwa hujazipata taarifa hizi tembelea
 mwenyewe kwenye tovuti husika (www.ajira.go.tz)

Friday, February 21, 2014

TAZAMA KWA URAHISI KABISA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 KUPITIA HAPA KING STAR BLOG!

Click hapa uangalie mdogo wako kapata division ngapi,au km n ww ndio mhusika mkuu jaribu kuvisit kingstar blog ili ujue umescore ngp! sitaki mtu azimie lakini!.....

fMATOKEO CSEE 2013
fMATOKEO QT 2013
fTANGAZO CSEE 2014

HAYA MASUALA YA TEKNOLOJIA BWANA!...USHAIONA HII?.....

HUHITAJ PASSPORT TENA KUSAFIRI NDANI NA NJE YA AFRIKA MASHARIKI.


You don’t need passport to travel all over East Africa



President Uhuru Kenyatta flanked by Deputy President William Ruto is shown a demonstration of the use of National Identity card for free movement within the East African Countries by Immigration officer Gladys Kang'ethe shortly before departing J.K.I.Airport for an official visit to Uganda. President Kenyatta exited Kenya and entered Uganda using his national identity card as a demonstration that East Africans do not require a passport or visa to travel to the regional states. PHOTO/PSCU

By NATION TEAM
In Summary
  • Many Kenyans, Burundians, Rwandans, Tanzanians and Ugandans are unaware that they do not require visas to travel to each others’ countries.
  • The East African Passport may be used for travel within the community only. It has a six-months multiple entry validity, which is one of the privileges it accords the holder.


President Kenyatta on Wednesday exited Kenya and entered Uganda using his national identity card as a demonstration that East Africans do not require a passport or visa to travel to the regional states.

The Kenya Airways plane carrying President Kenyatta and his entourage left Jomo Kenyatta International Airport shortly before 5pm.

This was meant to promote the movement of people and goods within the East African Community states without a passport or visa.

Many Kenyans, Burundians, Rwandans, Tanzanians and Ugandans are unaware that they do not require visas to travel to each others’ countries.

Although East Africans can use national passports to travel in the region, those without can use their national IDs.

The East African Passport may be used for travel within the community only. It has a six-months multiple entry validity, which is one of the privileges it accords the holder.

Certificates of identity or inter-state passes are issued by local immigration authorities to citizens who cannot be readily issued with a passport in emergency situations to travel across East Africa in place of a passport.

The common market protocol provides for the use of a machine readable national Identity Card for travel within the East African region, but only for citizens of those partner states which have accepted among themselves the use of such.

East African Community, Commerce and Tourism Cabinet Secretary Phylis Kandie said the introduction of a single visa for East Africans will help ease movement of goods and services across borders.


You don̢۪t need passport to travel all over East Africa - News - nation.co.ke
                                                       


KABINTI SPECIAL YA DULLY SYKES YAFUNGIWA.

Wote tumemsikia Prince Dully Sykes akiongelea kufungiwa kwa video yake ya kabinti special na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) . Kuna sababu kuu mbili zilizosababisha video hii kufungiwa na ya kwanza  ni kitendo cha msanii Diamond Platnumz kuvaa T-shirt iliyoandikwa neno ambalo ni tusi  . Hii ingekua kwa nchi za mbele basi ungekutwa t-shirt hii wanaifanyia kitu kinaitwa “blurring” yaani
wanayafanya maneno yasisomeke lakini wabongo wakaona isiwe tabu na director akaamua kuacha video irushwe ikiwa katika hali hii.Sababu ya  pili ni vazi la ufukwe yule demu alilovaa kitu ambacho dully ameona haikua mbaya.

Je unadhani basata wamefanya haki kuifungia hii video au ni miyeyusho tu!

Monday, February 17, 2014

WASTARA APATA AJALI TENA!....


MAJANGA! Siku chache baada ya hivi karibuni kudaiwa kunywa sumu, staa mkubwa wa sinemaBongo, Wastara Juma amepata tena ajali mbaya.Habari za uhakika zilizolifikia gazeti namba wani la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita zilieleza kuwa siku ya tukio Wastara alitoka nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar na gari lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili ya kwenda kununua umeme.
Akizungumzia tukio hilo kwa masikitiko, Wastara aliliambia gazeti hili kuwa kabla ya kufika kwenye kituo cha kununulia umeme (Luku) alikutana na lori kubwa lililokuwa kwenye mwendo kasi huku likiwa limewasha taa fulu.Alisema kuwa alijaribu kulikwepa lakini lilimsukuma na kujikuta akiingia mtaroni kutokana na barabara kuwa nyembamba ambapo aliumia sehemu za kichwani na mguuni kwa ndani.
Wastara alisema baada ya hapo alikimbizwa katika Hospitali ya TMJ, Dar ambapo alisafishwa majeraha (dressing) kisha akapatiwa matibabu na baadaye aliruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nimenusurika kifo, namshukuru sana Mungu kwani ajali ilikuwa mbaya nilihamishwa kwenye siti niliyokuwa nimekaa na kurushwa kwenye siti nyingine huku nikijigonga na kuumia kichwani.“Pia gari langu limeharibika sana, kioo chote kimevunjika, sielewi kwa nini haya yote yananitokea.
“Namuomba Mungu anisaidie maana naona mambo yanakwenda ndivyo sivyo na kwa nguvu zangu mwenyewe siwezi,”alisema Wastara.
Hata hivyo, Wastara kwa sasa anaendelea vizuri japokuwa bado anaumwa kichwa na mguu.
Wastara ameshapata ajali mara kadhaa ikiwemo ile ya pikipiki aliyopata mwaka 2008 akiwa na aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi akatwe mguu wa kulia. Pia aliwahi kupata nyingine ya gari akiwa na Sajuki.
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Wastara, kuna watu wanamtakia mabaya ili amfuate Sajuki aliyefariki Januari 2, mwaka jana.

DIAMOND HAWEZI KUNIPATA MIMI KABISA:MWANADADA AMISA AYATAMKA HAYA


MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la Miss Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa  mwanamuziki huyo ni shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema alistaajabu kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.

“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu

Sunday, February 16, 2014

EB WACHEKI HAWA WATOTO!



Kwa uzoefu wako ulionao unahisi hawa watoto watakuwa wanatokea mkoa gani hapa tanzania?





KIKWETE:UNYONGE CCM BASI


03_ecd2e.jpg

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge na kusema uvumilivu una kikomo chake.
Aliyasema hayo jana wakati anafungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, kilicholenga kuweka msimamo wa chama kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ambayo inaanza kujadiliwa Jumanne wiki ijayo.
"Tuna uchaguzi mdogo, Iringa, Kalenga, tumeshapata mgombea na tumefanya hiyo kazi kwa niaba yenu kwa sababu hatukupata muda wa kuitisha Kikao cha Halmashauri Kuu, lakini mmetupatia mamlaka ya kufanya hivyo na Katiba imetupa fursa ya kufanya uteuzi kwa niaba yenu,"alisema.
CCM imemteua Godfrey Mgimwa ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Dk William Mgimwa, kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu. Dk Mgimwa hadi anafariki dunia alikuwa Waziri wa Fedha.
Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na Chadema vikiwa vimetaja wagombea wake, Chadema kikiwa kimetangaza, Grace Tendega Mvanda.
Rais Kikwete alisema chama hicho kinashindana na vyama vingine katika uchaguzi huo mdogo.
"Tunashindana na wenzetu wagomvi, maana wao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa,"alisema Kikwete bila kutaja chama chochote cha siasa kwa jina.
"Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge," alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa Nec.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
"Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na mwache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake," alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.
"Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,"alisema.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa CCM kujipanga vizuri katika uchaguzi huo, ili kuhakikisha wanapata ushindi mnono.
"Mpaka sasa kwa dalili tulizonazo hatuna mgawanyiko wala hakuna misukosuko maana lile la Arumeru (uchaguzi mdogo katika Jimbo la Arumeru Mashariki) lilikuwa na misukosuko tangu tumeanza hadi tumemaliza," alisema.
Katika uchaguzi huo, uliofanyika Aprili mosi, 2012 mgombea wa Chadema, Joshua Nassari aliibuka mshindi baada ya kumshinda Sioi Sumari wa CCM ambaye ni mtoto wa marehemu Jeremiah Sumari, aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi mwaka 2008 hadi 2010.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na wanachama wa CCM katika kata 23, ambazo CCM iliibuka na ushindi na kuwataka kuweka nguvu zaidi katika kuzikomboa kata nne zilizoangukia mikononi mwa wapinzani.
Kata ambazo wapinzani walishinda ni Sombetini (Arusha Mjini), Kiboroloni (Moshi Mjini), (Njombe Mjini),zote zilichukuliwa na Chadema. Kilelema mkoani Kigoma (NCCR Mageuzi).
Aidha, Rais Kikwete alisema awali wakati wanaahirisha kikao cha Nec kilichopita, walikubaliana watakuwa wakihamia mikoani kufanya vikao hivyo ambapo Mbeya waliomba kuwa wenyeji na walikubaliwa.
Hata hivyo, alisema waliamua kufanya tena kikao hicho mjini hapa, kwa sababu ya agenda watakazozizungumza kwenye kikao hicho ambazo ni suala linalohusu mchakato wa Katiba Mpya.
"Ili tutakapoyamaliza, tujue tuweke misimamo gani itakayokwenda kwenye Bunge la Katiba. Haina maana kuwa ile agenda yetu ya Mbeya tumeifuta, ahadi iko palepale, kikao kitakachofuata cha kawaida kitafanyikia Mbeya,"alisema.
Awali Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimkaribisha Rais Kikwete, alisema kuwa wajumbe wa Nec ni 372, lakini waliohudhuria walikuwa ni 368 (sawa na asilimia 98.3) hadi kikao kinafunguliwa
                                                                 fkm!


Friday, February 14, 2014

PENDA KUTAKA KUJUA NINI KINAENDELEA NDANI NA NJE YA NCHI YAKO NA DUNIA NZIMA KIUJUMLA

Kwa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayotokea kila siku tembelea kingstar blog! Hii ni blog itakayokuwezesha wewe mtembeleaji kupata taarifa mbalimbali zinazotokea ndani na nje ya nchi!
kaa tayar kwa habar motomoto zitakazo kuelimisha,kuburudisha na kukufurahisha pia.....