Caf wamruhusu Okwi kuivaa Al Ahly
Hans Mloli na Khadija Mngwai
SHIRIKISHO la Soka Afrika (Caf), limemhalalisha mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi kuitumikia klabu yake hiyo rasmi kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuituma leseni yake nchini.

Awali, leseni ya mchezaji huyo raia wa Uganda, ilizuiwa na shirikisho hilo lenye makao yake makuu nchini Misri kutokana na utata wa awali juu ya usajili wa mchezaji huyo.
Caf ilituma leseni za wachezaji 25 watakaoitumikia klabu hiyo kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa huku jina la Okwi likisalia wakisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya TFF kuomba kujiridhisha juu ya usajili wa mchezaji huyo akitokea SC Villa ya Uganda.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, tayari leseni ya Okwi imeshatumwa na sasa yupo huru kuichezea Yanga kwenye michuano hiyo ya kimataifa.
“Leseni ya Okwi imeshatumwa, yupo tayari sasa kuichezea Yanga kwenye mashindano ya kimataifa, nafikiri leo (jana) baadaye au kesho (leo) tutawatumia taarifa rasmi Yanga kuhusiana na suala hili,” alisema Mwesigwa.

Kukwama kwa leseni hiyo, kulisababisha Okwi kukosa michezo miwili ya awali ya michuano hiyo dhidi ya Komorozine ya Comoro ambapo sasa ataanza kuitumikia Yanga kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar, Machi Mosi, mwaka huu.
Kwa upande wake Okwi aliyecheza mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na Yanga juzi Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting na kuonyesha uwezo mzuri, amesema amejiandaa vyema dhidi ya Aly Ahly ya Misri.
Kwa upande wake Okwi aliyecheza mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na Yanga juzi Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting na kuonyesha uwezo mzuri, amesema amejiandaa vyema dhidi ya Aly Ahly ya Misri.
Yanga inatarajia kukutana na Al Ahly Machi Mosi, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa jijini Dar.
Yanga ilifanikiwa kuingia hatua ya pili baada ya kuiondoa Komorozine ya Comoro kwa idadi ya mabao 12-2 nyumbani na ugenini.
Yanga ilifanikiwa kuingia hatua ya pili baada ya kuiondoa Komorozine ya Comoro kwa idadi ya mabao 12-2 nyumbani na ugenini.
“Namshukuru Mungu kuweza kufanikiwa kucheza na tumejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo unaofuata, naamini tutafanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu.
“Tunajua Al Ahly ni timu nzuri na ni ya kiushindani, hivyo tunahitaji kujipanga ili tuweze kufanikiwa kufanya vizuri katika mchezo huo na mechi nyingine za ligi.
“Siwezi kuzungumza kuhusu Simba kunizuia kutocheza kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Yanga hivi sasa na ninataka kuitumikia Yanga na siwezi kuizungumzia timu ambayo sipo kwa sasa,” alisema Okwi.
“Siwezi kuzungumza kuhusu Simba kunizuia kutocheza kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Yanga hivi sasa na ninataka kuitumikia Yanga na siwezi kuizungumzia timu ambayo sipo kwa sasa,” alisema Okwi.
No comments:
Post a Comment