Friday, May 16, 2014

TATIZO LA MAJI SUA LAANZA KUWA KERO KWA WANACHUO HAO. TAZAMA HAPA...

Kila mmoja anafahamu kwamba 'maji ni uhai' kwa kuwa anatambua umuhimu wa maji katika shughuli zetu za kila siku. Hali huwa tofauti kwa wanafunzi wa SUA kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo mara kadhaa hapo chuoni kwao. Hawa unaowaona hapa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha SOKOINE (SUA) wakiwa katika purukushani za kupata maji pindi yalipokuwa yamerudi.
 Tatizo hili huwa linatokea mara nyingi sana hapo chuoni na kuwafanya wanafunzi hawa wakazi wa New hostel kupoteza muda wao mwingi na kukwamishwa kwa baadhi ya shughuli zao za muhimu wakiwa wanasubiri maji yatoke au wakiwa kwenye foleni kubwa pale maji yanapoanza kutoka.
Sasa jiulize mwenyewe 'ziko wapi mamlaka za kushughulikia jambo hili' ili hawa wataalamu wetu wa baadae waweze kusoma katika mazingira mazuri yatakayo wavutia na kuwahamasisha wasome kwa bidii kwa ajili ya taifa letu la sasa na la baadae?
Na huu ndio mwonekano wa majengo hayo ambayo yanakabiliwa na tatizo hili. Ni vema utawala wa chuoni hapo ukaliona jambo hili na kulitatua mapema iwezekanavyo kwani huduma bora huleta ufanisi katika shughuli zetu za kila siku..

No comments:

Post a Comment