Tuesday, September 30, 2014

EBOLA:UNYANYAPAA WAONGEZEKA AFRIKA MAGHARIBI

Shirika la Unicef linahofia kuwa idadi ya mayatima walioondokewa na wazazi wao kutokana na Ebola itaongezeka
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takriban watoto elfu tano nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone, wamepoteza mzazi mmoja au wawili kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Shirika la umoja huo la kuwahudumia watoto, UNICEF, linasema kuwa kupata watu wa kuwahudumia watoto hao imekuwa vigumu sana kwa sababu ya unyanyapaa unaotokana na ugonjwa huo.
Shirika hilo linasema kuwa baadhi ya watoto, wanalishwa na majirani, lakini wakati mwingi hawana watu wa kuwajali.
Kadhalika shirika hilo limetoa mfano wa mtoto mmoja mdogo mwenye umri wa miaka minne kuondokewa na wazazi wake wawili.
Mtoto huyo alikuwa anasaidiwa na mwathiriwa wa Ebola lakini mpango mzima huo ulikosa kufaulu hasa baada ya mtoto huyo kunyanyapaliwa na jamii nzima.
Watoto walipatikana wakiwa wametelekezwa hospitalini ambako wazazi wao walifariki au majumbani ambako ikiwa wana bahati wanalishwa na majirani zao ila kwa kutengwa.
''Maelfu ya watoto wanakabiliwa na hatari kubwa baada ya kuondokewa na mama au baba au familia nzima kutokana na Ebola,'' alisema afisaa mmoja wa shirika la Unicef Manuel Fontaine.
Idadi ya mayatima katika kipindi hiki cha Ebola ni wengi sana na idadi hiyo imeongezeka kulingana na ripoti nyingine zikisema kuna hofu kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka ifikapo mwezi Oktoba.
Unicef inasema kuna haja kubwa ya kuwepo mfumo wa kuwatunza watoto hao.
BBC...

Monday, September 29, 2014

GARI ALILOZAWADIWA WEMA SEPETU JANA KWENYE SIKU YAKE YA KUZALIWA.




Hivi ndivyo alivyo kaririwa Diamond Katik Ukurasa wake wa siku ya jana..

"Nilitamani Nikupe vingi huenda ingesaidia kuelezea ni kiasi gani Nakupenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kizaliwa..
Lakini tu sina Uwezo huo mumy...
Tafadhari pokea kidogo Hichi nilicho jaaliwa leo..
Na siku zote tambua kwamba your Plutnum Love you so much.
Happy Birthday Baby."


hiki ndicho alichokisema mwanadada zamaradi kuhusiana na zawadi hiyo BIRTHDAY YA MWAKA!!!!!!!!! Hizi ndio zawadi kubwa alizopata WEMA leo.... NISSAN MURRANO na BMW moja kali hatari NYEUPE!!!! Asante mmanyema mwenzangu @diamondplatnumz umefunga watu midomo kudaadeki!!!! Hiyo nyeusi hapo ndio zawadi aliyotoa Diamond kwenda kwa @wemasepetu na zaidi alieleta Kukabidhi ni MAMA DIAMOND!!! how sweeeeeet..... haya sijui jipya lipi tena hapa la kuongea!!! 
Utaniazimaga kamoja wema niwe nacruise nipumzishe kidogo kibenzi changu.. lol #kidding HAPPY BIRTHDAY MY DARLING!!!!!!! Unastahili kila kitu!!!repost

 

Friday, September 26, 2014

MCHINJAJI WA I.S ATAMBULIWA.

Mkurugenzi wa FBI James Comey

Mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye huficha sura yake ambaye ni muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati akiwachinja mateka watatu kwenye video inayo nadi wanamgambo wa dola ya kiislam IS.
Pamoja na hayo Bwana Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja jina lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya mji wa London, na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa marafiki wa kimataifa.
Muuaji huyo wa waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa kujitolea David Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye mitandao na wanamgambo hao wa dola ya kiislam na kusaidia kufanya maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa jihad.
BBC..

Tuesday, September 9, 2014

MVUA NDOGONDOGO ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR ZALETA MAAFA.


Hapa ni mtaa wa lumumba jirani kabisa na kipata street ambapo barabara za ndani hazijawekwa lami hivyo kutokana na mvua ndogo inayonyesha barabara hizo zinaharibika kiasi cha kuleta shida kidogo katika usafiri.


Picha kwa hisani ya kingstar entertainment..

Sunday, September 7, 2014

Friday, September 5, 2014

KIONGOZI MKUU WA AL SHABAAB AUAWA.


Taarifa kutoka idara ya ulinzi ya Marekani Pentagon zinasema kuwa naibu mwanzilishi wa kundi la Al Shabaab Ahmed Godane ameuawa.

Source:bbc swahili..

OMG: AJALI MBAYA IMETOKEA HUKO MUSOMA LEO.NI AJALI MBAYA SANA.



Ajali kubwa sana imetokea huko musoma leo,ni mabasi mawili yamegongana uso kwa uso!!! Hadi sasa watu zaidi ya #34 wameripotiwa kufariki dunia papo hapo!!!
Na majeruhi ni #83.Inasikitisha sana kwani nimeshindwa kuposti hata picha za majeruhi,,

Monday, September 1, 2014

HALI IMEKUWA TETE KARIAKOO - MGOMO WAZUKA TENA KUHUSU MASHINE ZA EFD..


 Mgomo wa wafanyabiashara kuhusu kupinga makato yanayofanywa na serikali kupitia mashine za efd umeanza tena leo ambapo wafanyabiashara karibu wote wamegoma kufungua maduka yao.Hali imekuwa tete kwa baadhi ya wateja wanaotoka mikoani kwani wamefika dar na kukosa mahitaji yao waliyokuwa wanayahitaji.


 Baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara wengi wao walisema kwamba sio maana kwamba hawazitaki hizo mashine za efd bali wanataka mfumo uliowekwa kwenye hizo mashine ubadilishwe kwani unamnyonya mfanyabiashara kwa makato ya asilimia kama 18% hivi.
Jambo jingine walilolizungumzia ni kwamba mashine hizo haziangalii mfanyabiashara anapata faida kiasi gani ndio akatwe bali mashine hizo zinaangalia tu mapato unayopata katika kipindi fulani cha biashara jambo ambalo wanasema ni unyonyaji kwao wafanyabiashara.

Share na wenzako ili wapate kufahamu jambo hili kwa undani zaidi ili watu wapate sababu za kugoma na sio  tu kusema kwamba 'hatutaki mashine za efd' kwani hiyo njia haitatusaidia.