Mgomo wa wafanyabiashara kuhusu kupinga makato yanayofanywa na serikali kupitia mashine za efd umeanza tena leo ambapo wafanyabiashara karibu wote wamegoma kufungua maduka yao.Hali imekuwa tete kwa baadhi ya wateja wanaotoka mikoani kwani wamefika dar na kukosa mahitaji yao waliyokuwa wanayahitaji.
Baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara wengi wao walisema kwamba sio maana kwamba hawazitaki hizo mashine za efd bali wanataka mfumo uliowekwa kwenye hizo mashine ubadilishwe kwani unamnyonya mfanyabiashara kwa makato ya asilimia kama 18% hivi.
Jambo jingine walilolizungumzia ni kwamba mashine hizo haziangalii mfanyabiashara anapata faida kiasi gani ndio akatwe bali mashine hizo zinaangalia tu mapato unayopata katika kipindi fulani cha biashara jambo ambalo wanasema ni unyonyaji kwao wafanyabiashara.
Share na wenzako ili wapate kufahamu jambo hili kwa undani zaidi ili watu wapate sababu za kugoma na sio tu kusema kwamba 'hatutaki mashine za efd' kwani hiyo njia haitatusaidia.
No comments:
Post a Comment