Friday, October 17, 2014
KINACHOENDELEA KATI YA BOKO HARAMU,SERIKALI NA WANAFUNZI WALIOTEKWA NYARA.
Serikali ya Nigeria inasema kuwa
imefikia makubaliano na kundi la
wapiganaji wa Boko Haram kuhusu
wasichana waliotekwa nyara wa
Chibok.
Mkuu wa jeshi la Nigeria Alex
Badeh,aliyefichua makubaliano hayo
mwishoni mwa mkutano wa siku tatu
kati ya nchi hiyo na Cameroon
anasema kuwa wanajeshi wa Nigeria
watatimiza matakwa ya makubaliano
hayo.
Serikali imesema imekuwa ikifanya
mazungumzo na viongozi wa Boko
Haram.
Kulingana na afisaa mkuu kiatika ofisi
ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan
Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo,
wajumbe wa serikali walikutana na
wapiganaji wa Boko Haram mara
mbili nchini Chad chini ya uongozi
wa Rais wa Chad Idris Derby.
Alisema kuwa Boko Haram
wamekubali kuwaachilia huru
wasichana waliotekwa nyara mjini
Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu
kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika
mkutano mwingine utakaofanyika wiki
ijayo mjini Njamena.
Pia alieleza kwamba maafisa wa
ujasusi wa Chad walihusika katika
mpango huo na kwamba
wamethibitisha mazungumzo hayo
yamefikiwa na kukubalika na kiongozi
wa Boko Haram, Abubakar Shekau.
bbc....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment