Monday, December 15, 2014
HII HAPA HATIMA YA YULE YAYA MTESAJI UGANDA.
Yaya wa Uganda aliyejipata pabaya
kwa kumchapa mtoto wa mwajiri
wake, amehukumiwa jela miaka minne
kwa kosa la kumtesa mtoto.
Kisa cha yaya huyu kilizua hasira
miongoni mwa watu wengi katika
mitandano ya kijamii pale kanda ya
video iliibuka mitandaoni
ikimwonyesha yaya huyo akimchapa na
kumkanyaga mtoto mwenye mwaka
mmoja unusu.
Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa
miaka 22, alinaswa kwa kamera ya siri
akionekana akimchapa na kumkanyaga
mtoto huyo pamoja na kumzaba kofi.
Mnamo siku ya Ijumaa, Jolly alikiri
kumshambuilia mtoto akisema alikuwa
analipiza kisasi kwani mamake mtoto
huyo naye alikuwa amezoea
kumchapa.
Hata hivyo mama huyo alikanusha
madai ya Jolly ambaye polisi
walikuwa wamesema wangemshitaki
kwa kosa la jaribio la mauaji ila
kiongozi wa mashitaka akasisitiza
kuwa ingekuwa vigumu kuthibitisha
hilo.
Hakimu mkuu Lillian Buchan aliambia
Tumuhirwe kwamba alitenda uhalifu
ambao hauna hata kisingizio.
Alisema adhabu aliyompa inamtosha
kulingana na makosa yake kwa
kumtesa mtoto ambaye hana hatia.
Babake mtoto huyo, Eric Kamanzi
alisema aliweka kamera ya siri
nyumbani kwake baada ya kuwa na
shauku kumhusu mfanyakazi huyo.
Kanda ya video iliyomuonyesha Jolly
akimtendea unyama mtoto, ilitoka
kwenye kamera ambayo Bwana
Kimanzi aliweka nyumbani kwake
baada ya kushuku kuwa mtoto wake
alikuwa anatendewa unyama na pia
baada ya kumpata mtoto wake akiwa
na alama za majeruhi mwilini mwake.
Alimshitaki mwanamke huyo kwa
polisi na kisha kuisambaza kanda hio
kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu kutolewa,Kamanzi
alisema: "sio juu yetu kuamua adhabu
anayofaa kupewa Jolly. ''
"tunatumai kuwa hili ni funzo kwa
wafanyakazi wengi wa nyumbani
kwamba huwezi tu kwenda kwa
nyumba ya mtu na kumtesa mtoto na
kutarajia kuondoka tu kama
ulivyoingia. ''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment