Watoto wawili ambao ni ndugu wamefariki dunia katika kanisa la ufufuo na uzima,linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es salaam.
Watoto hao walifariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakiwa katika ibada juzi jumapili wakati watoto hao wakiwa na waumini wengine wakifuatilia ibada ya kufunga ndoa.
Inadaiwa kuwa watoto hao walipigwa na shoti baada ya kukanyaga nyaya za umeme wakati waumini waliponyanyuka kwenda kuwapokea maharusi wakati wakiingia kanisani hapo.
Baba mzazi wa watoto hao David Oturo ameonyesha hali ya wasiwasi ya kutokukubaliana na mazingira ya vifo vya watoto wake Sara mwenye miaka 10 naGudluck mwenye miaka minne na kusema ni vifo vya utatanishi.
Alisema siku hiyo kulikuwepo na watoto wengi waliokusanyika katika viwanja vya kanisa hilo lakini ni watoto wake waliofikwa na mauti hayo.
Aliongeza kuwa kabla ya kufikwa na mauti hayo majira ya mchana Sara aling’atwa na nyuki sehemu ya mguu ambao walitokea katika kanisa hilo gafla.
Alisema jioni ndipo watoto hao walipopigwa na shoti na baada ya kuangalia nyaya hizo hazikuwa zimechunika sehemu yoyote wala kuwa na dalili ya hitilafu.
Source;millardayo!
No comments:
Post a Comment