Friday, August 21, 2015

KIKOSI KIPYA CHA WACHEZAJI WALIOITWA TAIFA STARS.



Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars  Charles Boniface Mkwasa August 21 ametangaza kikosi cha wachezaji 22 watakaosafiri kwenda kuweka kambi ya siku 8 Istanbul UturukiMkwasa ametangaza kikosi hicho ambacho kila mchezaji aliyeitwa anatakiwa kuripoti saa 5 asubuhi siku ya Jumapili August 23 tayari kwa safari usiku wake.
Taifa Stars inakwenda kuweka kambi Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kuwania kucheza AFCON 2017, mechi ambayo itachezwa Septemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, orodha hiyo ya wachezaji 22 imetangazwa kutoka katika kikosi cha awali kilichotangazwa wiki mbili mbili nyuma.
Wachezaji walioitwa ni:
All Mustafa (Yanga SC)
Aishi Manula (Azam FC)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Shomari Kapombe (Azam FC)
Abdi Banda (Simba SC)
Mohamed Hussein (Simba SC)
Hassan Isihaka (Simba SC)
Juma Abdul (Yanga SC).
Haji Mngwali (Yanga SC).
Kelvin Yondani (Yanga SC).
Nadir Haroub (Yanga SC).
Mudathir Yahya (Azam FC)
Himid Mao (Azam FC)
Frank Domayo (Azam FC)
Salum Telela (Yanga SC)
Deus Kaseke (Yanga SC)
Said Ndemla (Simba SC)
John Bocco (Azam FC)
Farid Musa (Azam FC)
Rashid Mandawa (Mwadui FC)
Simon Msuva (Yanga SC)
Ibrahim Ajib (Simba SC.

Sunday, August 16, 2015

HII NI NYINGINE TENA KUHUSU LOWASSA NA WAFUASI WA UKAWA.

Jeshi la polisi jiji Mwanza limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda ukawa ili wasiandamane kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza kumpokea mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, anayetarajiwa kuwasili jijini huko kusaka wadhamini
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles mkumbo, amesema mabomu hayo yametumika ili kuwazuia wafuasi hao wasiweze kujazana uwanjani hapo na kusimamisha shughuli nyingine.

Saturday, August 1, 2015

MAELEZO YA NAPE NNAUYE KUHUSU KUCHUKULIWA KWAKE NA ASKARI WA TAKUKURU.


Gazeti la MWANANCHI limeandika HAPA kwamba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amefafanua ishu yake ya kuchukuliwa na askari wa Takukuru kwa mahojiano muda mfupi baada ya kuchukua fedha benki huko Lindi.
Nape anayewania ubunge wa Jimbo la Mtama, jana mchana aliamriwa na maofisa wa Takukuru kufika ofisi zao baada ya kutoka kuchukua fedha benki ya NMB eneo la Misonobarini mkoa Lindi.
Ninadhani hawa jamaa walipotoshwa. Mimi nimekwenda zangu benki kuchukua fedha, lengo langu ni kuwalipa mawakala,” alisema Nape jana jioni alipopigiwa simu na Mwananchi kutoa ufafanuzi na akaongeza kwamba “Wakaja hawa jamaa, wakajitambulisha kuwa wanatoka Takukuru, wakaniuliza ‘mbona ninachukua fedha nyingi kipindi hiki?’ Nikawaambia ‘nakwenda kulipa mawakala, na fedha zenyewe ni hizi Sh3.6 milioni
‘Basi, tukatoka taratibu tukaenda ofisini kwao, ni karibu tu na benki. Wakanihoji hata haikumalizika nusu saa, niliwaambia nataka kulipa mawakala wangu, tena fedha zenyewe hazitoshi, wako zaidi ya 100′ – Nape Nnauye
Nape aliongeza kusema kuwa walimkamata na akawaambia kuwa yeye ni mwadilifu >>> “Halafu ninyi, mnaacha marushwa makubwa makubwa huko, watu wanahonga halafu mnamvizia Nape masikini kwa Sh3mil?,” alisema.
Nape alielezea kufadhaishwa na tukio hilo akidai kuwa limetengenezwa kwa ajili ya kumchafua hasa kwa kuwa leo kuna kura za maoni lakini akasema anaamini yeye ni msafi ambapo Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Lindi, Stephen Chami alikiri kumhoji Nape lakini akasema walijiridhisha kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kulipa mawakala.

“Unajua tuna watu wetu, kwenye maeneo mbalimbali hasa kipindi hiki cha uchaguzi, tumeweka watu wetu maeneo mengi, tunataka kukomesha rushwa,”
Source-millardayo.