Gazeti la MWANANCHI limeandika HAPA kwamba Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amefafanua ishu yake ya kuchukuliwa na
askari wa Takukuru kwa mahojiano muda mfupi baada ya kuchukua fedha benki huko
Lindi.
Nape anayewania ubunge wa Jimbo
la Mtama, jana mchana aliamriwa na maofisa wa Takukuru kufika ofisi zao baada
ya kutoka kuchukua fedha benki ya NMB eneo la Misonobarini mkoa Lindi.
“Ninadhani hawa jamaa walipotoshwa. Mimi nimekwenda zangu benki
kuchukua fedha, lengo langu ni kuwalipa mawakala,” alisema Nape jana jioni
alipopigiwa simu na Mwananchi kutoa ufafanuzi na akaongeza kwamba “Wakaja hawa
jamaa, wakajitambulisha kuwa wanatoka Takukuru, wakaniuliza ‘mbona ninachukua
fedha nyingi kipindi hiki?’ Nikawaambia ‘nakwenda kulipa mawakala, na fedha
zenyewe ni hizi Sh3.6 milioni’
‘Basi, tukatoka taratibu
tukaenda ofisini kwao, ni karibu tu na benki. Wakanihoji hata haikumalizika
nusu saa, niliwaambia nataka kulipa mawakala wangu, tena fedha zenyewe
hazitoshi, wako zaidi ya 100′ – Nape Nnauye
Nape aliongeza kusema kuwa
walimkamata na akawaambia kuwa yeye ni mwadilifu >>> “Halafu ninyi,
mnaacha marushwa makubwa makubwa huko, watu wanahonga halafu mnamvizia Nape
masikini kwa Sh3mil?,” alisema.
Nape alielezea kufadhaishwa na
tukio hilo akidai kuwa limetengenezwa kwa ajili ya kumchafua hasa kwa kuwa leo
kuna kura za maoni lakini akasema anaamini yeye ni msafi ambapo Kamanda wa
Takukuru wa Mkoa wa Lindi, Stephen Chami alikiri kumhoji Nape lakini akasema
walijiridhisha kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kulipa mawakala.
“Unajua tuna watu wetu, kwenye
maeneo mbalimbali hasa kipindi hiki cha uchaguzi, tumeweka watu wetu maeneo
mengi, tunataka kukomesha rushwa,”
Source-millardayo.
No comments:
Post a Comment