Friday, July 25, 2014

HOSPITALI YA IMTU YAFUNGIWA NA SERIKALI.




Lile sakata la kunaswa kwa viungo vya binadamu zaidi ya 150 huko Bunju nje kidogo la jiji wa Dar es salaam limepelekea kufungiwa kwa hospital iliyohusika na utupaji huo(IMTU) ambayo pia inatoa mafunzo ya udaktari kwa wanafunzi wanaosomea fani hiyo hapo chuoni.
Chama cha madaktari kililaani sana kitendo hicho kwani ilisemekana kwamba ni ukiukwaji wa maadili na viapo vya fani hiyo.
Baada ya tukio hilo serikali ilifanya ukaguzi wa kushtukiza hospitalini hapo na kubaini mapungufu mengine mengi kama vile kukosa baadhi ya vifaa vya muhimu pamoja na kuchanganya dawa zilizopitwa na muda.Wanafunzi wa chuo hicho wapigwa na butwaa na uamuzi huo na kushindwa nini cha kufanya!.
kingstar!..

TAZAMA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAR 26 JULY.

DSC01150
DSC01151
DSC01152
DSC01153
DSC01154
DSC01155
DSC01157
DSC01158
DSC01159
DSC01160
DSC01162
DSC01163
DSC01175
DSC01176
DSC01164
DSC01165
DSC01167
DSC01168
DSC01169
DSC01170
DSC01171
DSC01172
DSC01173
DSC01174
DSC01178
DSC01179
DSC01180
DSC01181
DSC01182

Friday, July 18, 2014

HIVI NDIVYO KESI YA MUME WA FLORA MBASHA INAVYOENDELEA MAHAKAMANI.

7mbshMume wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo imeanza Mbasha hajapeleka wakili yoyote.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
6mbsh
3mbsh
millard ayo!

Wednesday, July 16, 2014

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA (ACSEE 2014).


 Tazama kwa urahisi kabisa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2014.Bonyeza linki ifuatayo kuyaangalia moja kwa moja kupitia blog yako hapa:
fMATOKEO ACSEE 2014
Kwa wale wanaotaka kuangalia matokeo ya ualimu 2014 fuata linki ifuatayo:
fMATOKEO UALIMU 2014

Wednesday, July 2, 2014

MPIGIE KURA DIAMOND PLATNUMZ ILI AWEZE KUSHINDA AFRIMMA AWARDS.

Baada ya BET tunalejea tena nyumbani Afrika, Diamond yupo nominated kwenye Tuzo za #Afrimma( AFRICAN MUSIC MAGAZINE AWARDS) awards,zitakazofanyika jijini Texas,tarehe 26 july.
Yupo nominated kwenye category 5.
Best male east afrika
Song of the year(number1).
Video of the year (number 1)
Best collabo (nymber1 rmx)ft davido
And Best afrikan artist of the year
.kuvote fuata link hii http://afrimma.com/afrimma-nominees-2014/
Kisha vote kwenye kila category aliyopo.

KURA yako ndiyo itakayomuwezesha diamond aweze kushinda tuzo hizi. Tusiwe watu wa kushangaa asipopota tuzo wakati hatupigi kura.
Link iyo apo sasa na kazi ni kwenu..

Thursday, June 19, 2014

TAARIFA NYINGINE KUHUSU KESI YA MUME WA FLORA MBASHA.


Mbasha 2
Hizi ni picha za leo Emmanuel Mbasha akiwa anafikishwa Mahakamani.
Hii ni taarifa ambayo ilianzia kusambaa kwenye simu watu kutumiana sauti za sehemu ya kilichotokea kwenye tukio, baadae ikaingia kwenye mitandao mbalimbali zikiwemo blogs na facebook, na sasa ni mpaka kwenye magazeti, Radio na TV.
Taarifa mpya za leo ni kwamba Emmanuel Mbasha anayekabiliwa na kesi ya kumbaka mdogo wa mke wake, ameachiwa leo kwa dhamana baada ya kutimiza masharti katika mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Kwenye masharti aliyotimiza Emmanuel ambae ni mume wa mwimbaji Flora Mbasha, ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao wote ni wafanyakazi katika taasisi inayotambulika kisheria.
Mbasha 3June 17 2014 mbele ya hakimu Willbaforce Rwago wa mahakama hiyo, mwendesha mashtaka wa serikali Nassoro Katuga alidai  kuwa mshatakiwa alitenda kosa hilo Mei 23 mwaka huu eneo la Tabata Kimanga.
Emmanuel Mbasha alifikishwa mahakamani hapo na kukana shitaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 anaedaiwa kuwa shemeji yake hivyo akarudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Mwendesha mashtaka wa serikali alieleza Mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na imepangwa kutajwa tena July 17 mwaka huu.
Mbasha 1
source:millard ayo!..

Monday, June 9, 2014

SABABU ZA JENIFFER LOPEZ KUTOPAFOMU KWENYE UFUNGUZI WA KOMBE LA DUNIA.

jennifer-lopez-pitbull-claudia-leitteMichuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuanza siku ya alhamisi wiki hii nchini Brazil kwa ufunguzi wa mechi kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia, lakini kama ilivyo kawaida kabla ya mechi husika ya ufunguzi kunakuwepo na sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo mikubwa. Mwaka huu wasanii Jennifer Lopez,  Claudia Leitte na Pitbull walipangwa kutumbuiza.
Lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba JLO amegoma kwenda kutumbuiza kwenye sherehe hizo za ufunguzi pamoja na kwamba ndio msanii alioimba wimbo rasmi wa michuano hiyo. 
Staa huyo ambaye wiki iliyopita ameachana na mpenzi wake Casper Smart – leo hii jina lake halikuwemo kwenye listi ya wasanii watakaosindikiza sherehe za ufunguzi alhamisi hii.
Kwa mujibu wa FIFA,  Jennifer Lopez hatotumbuiza kwenyey sherehe hizo kutokana na ‘sababu za kiufundi’ ambazo hazikufafanuliwa ni zipi.
Hata hivyo wasanii wengine walioshirikiana na JLO kuimba wimbo wa ‘Ole Ole’ – Pitbull na Claudia Leitte watapafomu kwnye sherehe hizo. 
millard ayo!

Monday, June 2, 2014

TAIFA STARS WAREJEA VEMA TANZANIA BAADA YA USHINDI MZITO.

9s4a0125
Kikosi cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu) kiliitupa Zimbabwe (Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka Harare.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia Nairobi.
Stars imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, kwani awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika raundi ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Wakati huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka kikwazo hicho cha kwanza katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Salamu hizo zimetoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.