Monday, January 25, 2016

HII HAPA TAARIFA YA MAHAKAMA YA MWANZA KUHUSU HUKUMU YA ESTHER BULAYA KUPINGWA UBUNGE




Uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais wa Tanzania ulifanyika October 25 2015, baada ya hapo matokeo yakatoka na kukawa na stori mfululizo kuhusu ishu ya matokeo ikiwemo Wabunge wengine waliofungua kesi Mahakamani kupinga matokeo.

Mmoja ya Wabunge ambao walifunguliwa kesi za kupingwa Ubunge Mbunge wa Bunda,Ester Bulaya nae alikuwa na kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza.

Kwanza ni kwamba Mahakama hiyo imefuta kesi hiyo, kingine ni kwamba Mahakama hiyo imesema waliofungua kesi hiyo ni wapigakura ambao hawana mamlaka ya kufungua kesi ya aina hiyo.
Source;Millardayo.

Thursday, November 19, 2015

HUYU HAPA WAZIRI MKUU ALIYETEULIWA NA RAIS JPM LEO.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Serikali ya


Dar es Salaam.
Rais John Magufuli leo amewasilisha bungeni jina la Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano.


Spika wa Bunge, Job Ndugai alipokea barua iliyotoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa watumishi wa chombo hicho cha kutunga sheria na baada ya kuifungua ndipo aliposoma ujumbe huo uliotaja jina la Majaliwa ambaye alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.


Baada ya tangazo hilo ambalo lilipokelewa kwa shangwe na wabunge wengi, Spika Ndugai aliahirisha bunge kwa dakika arobaini na tano kuwapa nafasi wabunge kutafakari uteuzi huo kisha kumthibitisha bunge litakaporejea.


Waziri Mkuu huyo mteule alizaliwa Disemba 22, 1960 na kupata elimu katika Shule ya Msingi Mnacho kati ya mwaka 1970-1976 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Kigonsera kati ya mwaka 1977- 1980.


Mwaka 1991-1993 alijiunga na Chuo Cha Ualimu Mtwara. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1994 na kuhitimu mwaka 1998 kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden kwa masomo ya juu.


Amehudumu katika nafasi mbalimbali tangu mwaka 1984 alipojiunga na utumishi wa umma kama mwalimu mkoani Lindi, Katibu wa Chama cha Waalimu Wilaya, Katibu chama waalimu Mkoa na Mkuu wa Wilaya.


Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kabla ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumteua mwaka 2012 kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.

Friday, August 21, 2015

KIKOSI KIPYA CHA WACHEZAJI WALIOITWA TAIFA STARS.



Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars  Charles Boniface Mkwasa August 21 ametangaza kikosi cha wachezaji 22 watakaosafiri kwenda kuweka kambi ya siku 8 Istanbul UturukiMkwasa ametangaza kikosi hicho ambacho kila mchezaji aliyeitwa anatakiwa kuripoti saa 5 asubuhi siku ya Jumapili August 23 tayari kwa safari usiku wake.
Taifa Stars inakwenda kuweka kambi Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kuwania kucheza AFCON 2017, mechi ambayo itachezwa Septemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, orodha hiyo ya wachezaji 22 imetangazwa kutoka katika kikosi cha awali kilichotangazwa wiki mbili mbili nyuma.
Wachezaji walioitwa ni:
All Mustafa (Yanga SC)
Aishi Manula (Azam FC)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Shomari Kapombe (Azam FC)
Abdi Banda (Simba SC)
Mohamed Hussein (Simba SC)
Hassan Isihaka (Simba SC)
Juma Abdul (Yanga SC).
Haji Mngwali (Yanga SC).
Kelvin Yondani (Yanga SC).
Nadir Haroub (Yanga SC).
Mudathir Yahya (Azam FC)
Himid Mao (Azam FC)
Frank Domayo (Azam FC)
Salum Telela (Yanga SC)
Deus Kaseke (Yanga SC)
Said Ndemla (Simba SC)
John Bocco (Azam FC)
Farid Musa (Azam FC)
Rashid Mandawa (Mwadui FC)
Simon Msuva (Yanga SC)
Ibrahim Ajib (Simba SC.

Sunday, August 16, 2015

HII NI NYINGINE TENA KUHUSU LOWASSA NA WAFUASI WA UKAWA.

Jeshi la polisi jiji Mwanza limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda ukawa ili wasiandamane kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza kumpokea mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, anayetarajiwa kuwasili jijini huko kusaka wadhamini
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles mkumbo, amesema mabomu hayo yametumika ili kuwazuia wafuasi hao wasiweze kujazana uwanjani hapo na kusimamisha shughuli nyingine.

Saturday, August 1, 2015

MAELEZO YA NAPE NNAUYE KUHUSU KUCHUKULIWA KWAKE NA ASKARI WA TAKUKURU.


Gazeti la MWANANCHI limeandika HAPA kwamba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amefafanua ishu yake ya kuchukuliwa na askari wa Takukuru kwa mahojiano muda mfupi baada ya kuchukua fedha benki huko Lindi.
Nape anayewania ubunge wa Jimbo la Mtama, jana mchana aliamriwa na maofisa wa Takukuru kufika ofisi zao baada ya kutoka kuchukua fedha benki ya NMB eneo la Misonobarini mkoa Lindi.
Ninadhani hawa jamaa walipotoshwa. Mimi nimekwenda zangu benki kuchukua fedha, lengo langu ni kuwalipa mawakala,” alisema Nape jana jioni alipopigiwa simu na Mwananchi kutoa ufafanuzi na akaongeza kwamba “Wakaja hawa jamaa, wakajitambulisha kuwa wanatoka Takukuru, wakaniuliza ‘mbona ninachukua fedha nyingi kipindi hiki?’ Nikawaambia ‘nakwenda kulipa mawakala, na fedha zenyewe ni hizi Sh3.6 milioni
‘Basi, tukatoka taratibu tukaenda ofisini kwao, ni karibu tu na benki. Wakanihoji hata haikumalizika nusu saa, niliwaambia nataka kulipa mawakala wangu, tena fedha zenyewe hazitoshi, wako zaidi ya 100′ – Nape Nnauye
Nape aliongeza kusema kuwa walimkamata na akawaambia kuwa yeye ni mwadilifu >>> “Halafu ninyi, mnaacha marushwa makubwa makubwa huko, watu wanahonga halafu mnamvizia Nape masikini kwa Sh3mil?,” alisema.
Nape alielezea kufadhaishwa na tukio hilo akidai kuwa limetengenezwa kwa ajili ya kumchafua hasa kwa kuwa leo kuna kura za maoni lakini akasema anaamini yeye ni msafi ambapo Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Lindi, Stephen Chami alikiri kumhoji Nape lakini akasema walijiridhisha kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kulipa mawakala.

“Unajua tuna watu wetu, kwenye maeneo mbalimbali hasa kipindi hiki cha uchaguzi, tumeweka watu wetu maeneo mengi, tunataka kukomesha rushwa,”
Source-millardayo.

Wednesday, July 1, 2015

SALAMA JABIR AZUNGUMZA HAYA KUHUSU VIDEO MPYA YA ALIKIBA.


salama jj

Mtangazaji wa Mkazi na jaji wa mashindani ya vipaji Tanzania [bss] Salama J ametoa mtazamo wake kwa mahache kupitia twitter kuhusu video mpya ya Ali Kiba ‘Chekecha Cheketua’. Soma Twit zake hapa.

salama 1

Kiukwel mashabiki wa muziki wa Tanzania tuache propaganda na longolongo zisizo na maana! Video ni kali so Big up kwa ALLY SALEH KIBA!...

Saturday, May 23, 2015

YA NKURUNZIZA MWACHIE MWENYEWE BWANA! EBU MUONE APA!

nziza2

Burundi kwa sasa iko kwenye vichwa vingi vya habari kutokana na hali ya machafuko inayoendelea nchini humo baada ya Raisi Pierre Nkurunziza kutangaza kugombea tena uraisi awamu ya tatu mfululizo!

nziza

Jaribio la kutaka kumpindua madarakani wakati akiwa Tanzania lilifeli na sasa uamuzi uliofikiwa ni kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge nchini humo.
      Jambo lingine lililowashangaza watu ni kuwa pamoja na hali ya machafuko inayoendelea nchini humo yeye ameonekana akiwa uwanjani akicheza mpira kwa raha zake.

nziza3

Pia inasemekana kwamba mtu mmoja amepigwa risasi na askari waliokuwa wakilinda usalama mjini bujumbura wakati maandamano yalipokuwa yakifanyika.

Tuesday, May 19, 2015

WATOTO 2 WAFA KANISANI KWA GWAJIMA.

Watoto wawili ambao ni ndugu wamefariki dunia katika kanisa la ufufuo na uzima,linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es salaam.
Watoto hao walifariki baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakiwa katika ibada juzi jumapili wakati watoto hao wakiwa na waumini wengine wakifuatilia ibada ya kufunga ndoa.
Inadaiwa kuwa watoto hao walipigwa na shoti baada ya kukanyaga nyaya za umeme wakati waumini waliponyanyuka kwenda kuwapokea maharusi wakati wakiingia kanisani hapo.
Baba mzazi wa watoto hao David Oturo ameonyesha hali ya wasiwasi ya kutokukubaliana na mazingira ya vifo vya watoto wake Sara mwenye miaka 10 naGudluck mwenye miaka minne na kusema ni vifo vya utatanishi.
Alisema siku hiyo kulikuwepo na watoto wengi waliokusanyika katika viwanja vya kanisa hilo lakini ni watoto wake waliofikwa na mauti hayo.
Aliongeza kuwa kabla ya kufikwa na mauti hayo majira ya mchana Sara aling’atwa na nyuki sehemu ya mguu ambao walitokea katika kanisa hilo gafla.
Alisema jioni ndipo watoto hao walipopigwa na shoti na baada ya kuangalia nyaya hizo hazikuwa zimechunika sehemu yoyote wala kuwa na dalili ya hitilafu.
Source;millardayo!