Monday, March 31, 2014

LIGI YA MABINGWA 2013-2014:TUMAINI LA MWISHO KWA MANCHESTER UNITED.

moyes_a46c5.jpg
Kocha wa Manchester United, David Moyes.
London, England.Manchester United, ambayo msimu huu inaonekana kupoteza nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, wiki hii itaanza kutupa kara zake za mwisho kwenye michuano hiyo wakati wa mechi za robo fainali zitakazochezwa kesho na keshokutwa kabla ya mechi za marudiano zitakazochezwa Aprili 8 na 9.
Karata hizo za Man U ni ngumu kutokana na ukweli kuwa inakutana na Bayern Munich kwenye Uwanja wa Old Trafford kabla ya kumaliza raundi hiyo kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Katika mechi nyingine Barcelona itaikaribisha Atletico Madrid kwenye Uwanja wa Camp Nou, Hispania.
Man United vs Bayern Munich
Mechi ya Man U na Bayern ni kumbukumbu ya fainali za mwaka 1999 ya Ligi ya Ulaya wakati Manchester iliposawazisha katika dakika ya mwisho na kufunga bao la pili lililoipa klabu hiyo kongwe ya Uloaya ubingwa wa pili wa Ulaya kwa kushinda kwa mabao 2-1.
Bayern Munich ilipata bao la kuongoza mapema katika dakika ya 6 lililofungwa na Mario Basler, lakini Manchester ilisawazisha dakika ya 90 kwa bao la Teddy Sheringham na kuongeza bao la pili dakika ya tatu ya majeruhi lililofungwa na Ole Gunnar Solskjaer.
Hata hivyo, katika mipambano mingine ya timu hizo katika hatua ya robo fainali msimu wa 2009/10 na 2000/01, Bayern iliibuka kidedea.
BarcelonaVs Atletco madrid.

WALIYOYASEMA MASHABIKI WA YANGA BAADA YA TIMU YAO KULAZWA BAO 2-1 NA MGAMBO JKT..

hamis_kiizakulia_akijaribu_kumtoka_beki_wa_azam,david_mwantikaLigi kuu ya Vodacom iliendelea wikiendi hii kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti nchini.
Mabingwa watetezi Yanga walikuwa katika dimba la Mkwakwani kukipiga na Mgambo, matokeo ya mchezo Yanga walipoteza mchezo wa jana kwa kipigo cha magoli 2-1, kipigo ambacho kimewashitua mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wakidai kwamba kuna mkono wa mtu.
Mashabiki hao ambao wengi wao walitoka Dar es Salaam,  walichanganyikiwa zaidi baada kusikia Azam FC imeipiga Simba mabao 2-1 jijini Dar es Salaam na kuwaacha kwa pengo la pointi saba kileleni katika mbio za kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Azam sasa imefikisha pointi pointi 53 ambazo zimewaweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza tangu iasisiwe Juni 24, 2007.
Yanga imebaki kwenye nafasi ya pili na pointi 46 huku Mbeya City ikifikisha pointi 45 na kuzidi kujikita nafasi ya tatu baada ya kuilaza Prisons bao 1-0 pia jana Jumapili na kufufua matumaini ya kuwania nafasi ya pili.
Pointi 53 zinaweza kufikiwa na Yanga au Mbeya City pekee. Matokeo ya Azam na Simba, yanawafanya Wekundu wa Msimbazi kubaki nafasi ya nne na pointi zao 36 baada ya mechi 23.
Mbeya City nao waliwashikisha adabu ndugu zao Prisons kwa kuwafunga 1-0 katika dimba la Sokoine Mbeya.
Coastal Union walifungwa 3-1 na Mtibwa Sugar. Kagera Sugar wakatoka sare na Ruvu Shooting.

Saturday, March 29, 2014

NDEGE YA MALAYSIA KUTAFUTWA ENEO JIPYA.

Ndege 9 za kijeshi na Moja ya kiraiya zinatafuta mabaki ya ndege ya Malaysia ya MH370
Maafisa wanaosaidia katika harakati za kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu yaliyopita , wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege hiyo.
Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja mia moja kazkazini mashariki mwa kusini mwa bahari hindi.
Mamlaka ya usalama wa baharini nchini Australia imesema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa Malaysia pamoja na matokeo ya utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.
Eneo inakotafutwa ndege ya Malaysia
Ndege hiyo iliyotoweka March tarehe 8 ikiwa na abiria 239 sasa inadaiwa kwamba ilikuwa katika mwendo wa kasi kinyume na ilivyokadiriwa na kwamba huenda iliishiwa na mafuta ghafla.
Meneja mkuu wa shirika la utafiti wa anga za juu ya Australia John Young, amesema utafiti mpya unaonesha kuwa ndege hiyo ya MH370 ilikwea juu na kufululiza kwa kasi mno na hiyo inaweza kuwa
sababu ya mafuta ya ndege hiyo kumalizika haraka.

Kutokana na hesabu hiyo mpya eneo la kutafutwa kwa ndege hiyo imehamishwa hadi umbali wa kilomita 1,850 Magharibi mwa Perth na itakuwa katika eneo lenye kilomita 319,000 mraba katika bahari Hindi.
                                                          By
                                                          King star!...

Wednesday, March 26, 2014

TUME YA WARIOBA YAVUNJWA RASMI.

kikwete_15d33.jpg
Rais Jakaya Kikwete ameivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba, baada ya kukamilisha kazi yake, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2013 katika Bunge Maalumu la Katiba wiki iliyopita.
Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni ya wananchi kwa zaidi ya miezi sita na hatimaye kuandaa rasimu ya kwanza na ya pili, ambayo inatarajiwa kuanza kujadiliwa katika Bunge hilo wakati wowote kuanzia sasa.

Tuesday, March 25, 2014

TAZAMA GARI JIPYA KABISA ALILONUNUA MASANJA MKANDAMIZAJI NA MANENO ALIYOYOYAANDIKA.



dd
Huu ndio usafiri mpya wa masanja mkandamizaji!

Sunday, March 23, 2014

UKIONA MAMBO KAMA HAYA YANATOKEA SANA KWENYE MAHUSIANO YENU UJUE KWAMBA HAKUNA ISHU TENA HAPO..

1.KILA ANACHOFANYA SIKU HIZI KINAKUBOA
Hii ikitokea maana yake ni nini???Hakuna analofanya kwako jema,kila anachojaribu kufanya whether its good for u lakini wewe inaku-piss off...Kuna jambo..Siku zote,mtu akikutoka rohoni,hakuna jema atafanya utaona..Hiyo ni dalili kwamba amekutoka moyoni..the love is dead...Ukimpenda mtu,utapenda mambo anayofanya,sometimes ni mabaya lakini you live with them because YOU ARE N LOVE.If what happens is the opposite,sepa!

2.HUPENDI VILE ULIVYOMPENDEA
Kama ulimpendea alivyo,Nywele,Macho,anything...Ghafla Personality ile iliyokuvutia imepotea..Huoni uzuri wake anymore,unaona karaha tu,,,hata avaeje unaona hapendezi,nywele nzuri zinaonekana minywele au kipilipili...Mama,sepa tu...You have lost ur appetite in him,u wont eat him no more

3.PRIORITIES ZENU ZINADIFFER

Hapa ndo patamu..Umewahi kuona Relationship zenye argument kwenye kila kitu???Mama anataka wali baba ugali...Mama anataka kujenga Baba anataka gari...Mama anawaza kutoka Outing Baba ana hamu ya kulala...Moja haikai 2 ndo kabisa haisimami....Mtawezaje kukaa pamoja huku mnatofautiana mitazamo????Ikifikia hapa,bora ujichenge fasta,ukikazana utaumia

4.HAUM-MISS AKIWA HAYUPO
Zamani akiondoka tu unatamani arudi...Haipiti siku hujamuona....You miss texting na kumcall..

Siku hizi wala,unakata wiki asipotaka kukuona unakausha tu na unaona fresh....Asipokupigia na kukutext na ww unasahau kabisa kama anaexist...That Love is dead

5.UNAONEA WIVU SANA WENZIO 
Ukiona unaona sana wivu kwa wenzako wenye relationship na kuhisi wanafaidi sana jua kwako kumezama..Kama kwako kungekuwa salama ungejisikia ur better off kuliko wenzio na hata kama wanafanya jambo romantic kwako si ajabu maana nawe unafanya...Dalili kwamba what they have kwako imekufa inakukoroga nafsi,unatamani zama zirudi ila ndo zimepita,ni kipimo tosha kwamba Penzi lako limekufa

6.UNAONA SANA NJE

Zamani hata pite mdada mcutie wala hukuwa na habari...Hata apite mkaka ananukia,unatembea kwa mguu unapewa Lifti wala huhangaiki...Ila siku hizi macho yamekutoka,Kikalio kidogo unakifuatilia kama taarifa ya habari ya BBC....Kila mkaka unaona Hes Cute,wow Hes cutee,,,Jua kwako kumeungua

7.MAGOMVI HAYAISHI
Kuna watu wanateteaga ugomvi..Kwamba bila ugomvi eti Relationship haigrow...Sawa!Lakini Kila saa??Kila Siku??Kugrow gani huko???Kila muda manundu,labda mnakuza ndonya!
Ukiona magomvi kila saa kwa vitu vya kiboya na kipuuzi,na haikuwa hivi zamani,Jiulize,KULIKONI???

8.UMECHEAT/UMEMKUTA ANACHEAT

Hii ndo funga kazi,huoni tabu kucheat...Hata akijua poa tu...Hiyo ni dalili kwamba Jumba Bovu limeegama upande....When ur in love, there must be some Guilty Conscious in You....Ikipotea hiyo  bhaaassssssssss..Ukiona manyoya ujue kaliwa!

ARSENAL WAADHIBIWA VIKALI NA CHELSEA..

-Ni katika mechi ya 1,000 kwa kocha Arsene Wenger

- Refa atoa kadi nyekundu kwa mchezaji asiyestahili

Arsenal wameonja kichapo kikali zaidi katika Ligi Kuu msimu huu, katika siku ambayo kocha wake, Arsene Wenger ametimiza mechi ya 1,000 na klabu hiyo.
Washika Bunduki wa London walionekana kuanzia mguu mbaya tangu mwanzo, waliporuhusu mabao mawili ya haraka kupitia kwa Samuel Eto’o na Andre Schurrle dakika ya tano na ya sita katika dimba la Stamford Bridge.
Alex Oxlade-Chamberlain alichupa dakika ya 17 na kupangua kwa vidole mpira uliokuwa ukikaribia lango kwa juu kana kwamba ndiye alikuwa kipa, lakini mwamuzi Andre Marriner akakosea na kumpa kadi nyekundu Kierran Gibbs.
Marine alishikilia msimamo huo licha ya Oxlade-Chamberlain kumweleza kwamba ndiye aliyeunawa mpira huku Gibbs pia akieleza hakuwa ameshika mpira huo. Wachezaji wa Arsenal pia walielekea kupinga lakini mwamuzi hakubadilisha uamuzi wake.
Kwa mpira kushikwa na mchezaji ndani ya eneo la penati, ilitolewa adhabu hiyo na Eden Hazard hakuwa na tabu yakuukwamisha mpira wavuni akimwacha kipa Wojciech Szczesny bila la kufanya na kuwa bao la tatu.
Kutolewa kwa Gibbs kulitoa mwanya kwa nahodha Thomas Vermaelen kuingia kwa gharama ya Mjerumani Lukas Podolski kwenda nje, na mafuriko yaliendelea kwa bao la dakika ya 42 la Oscar kasha wakaenda mapumziko.
Kipindi cha pili Arsenal hawakuweza kuuona mlango wa Chelsea, bali waliruhusu mabao mawili zaidi kupitia kwa Oscar katika dakika ya 66 na Mohamed Salah dakika ya 71. Huu ndio ushindi mkubwa zaidi wa Jose Mourinho ndani ya Chelsea na pia ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kuwafunga wenzao wa London kwa idadi kubwa hivyo ya mabao.
Wenger atataka kuisahau siku hii muhimu kwake, ambapo Chelsea walizidisha pengo la pointi dhidi ya Arsenal kutoka nne hadi saba. Bado Arsenal wana kibarua kizito dhidi ya Manchester City Jumamosi ijayo, lakini watacheza kwanza na Swansea Jumanne hii.
Wenger alijiunga na Arsenal 1996 na ndiye anayeongoza England kwa kudumu muda mrefu zaidi kwenye timu moja, baada ya kustaafu kwa Alex Ferguson wa Manchester United mwaka jana, baada ya kukaa hapo kwa miaka 26 na nusu.

TAZAMA PICHA ZA MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA.

*Mabaki ya ndege iliyopotea*

Picha za Satelite ambazo China inasema huenda ni mabaki ya ndege iliyopotea
China imeanza kuchunguza picha mpya za setilite zinazoonyesha kitu kama mabaki ya ndege kwenye eneo la kusini mwa bahari ya Hindi.
Picha hizo ni muhimu kwa ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea, maafisa wa Malaysia wanasema.
Kaimu Waziri wa Usafirishaji Hishammuddin Hussein amesoma taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa ambapo amesema kuna kitu kama mabaki ya ndege chenye ukubwa wa mita 30 kwa 22 kilichoonekana.
Amesema serikali ya China itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo baadae.
Ndege MH370 mali ya Shirika la ndege la Malaysia ilipotea kwenye masiliano ilipokuwa imeondoka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing march 8 ikiwa na abiria 239.

Friday, March 21, 2014

RAISI JAKAYA KIKWETE KULIHUTUBIA BUNGE MUDA HUU.


Picha hapo juu inamuonesha mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa safarini kutoka Dar es  salaam kuelekea Dodoma kwa ajili ya kulihutubia bunge.Hapo anaipitia hotuba yake ambayo ndio inatolewa muda huu,
            Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge maalumu la katiba kwa mujibu wa kanuni 7(1)g na kanuni 75(1) ya kanuni za bunge maalumu.
                    Picha na                                                                                                                                                       Ikulu                                                                                                              






PISTORIUS MWANARIADHA WA A.KUSINI KUUZA NYUMBA YAKE YA KIFAHARI.


Nyumba ya kifahari ya Oscar Pistorius
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorious atauza nyumba yake ili aweze kumudu gharama ya kesi ya mauaji inayomkabili.
Oscar hajaweza kurejea katika nyumba yake hata baada ya maafisa wa uslama kumruhusu arejee huko zaidi ya mwaka mmoja uliopita huku uamuzi ukitolewa wa nyumba ile kusalia ikiwa imefungwa hadi pale kesi hiyo itakapo kamilka.Hii ni kwa mujibu wa wakili wake Brian Webber ambaye amenukuliwa na Shirika la Wanahabari La Afrika Kusini (SAPA) akisema kesi hiyo itaendelea kwa zaidi ya wiki tatu zilizotarajiwa kwa kesi hiyo kukamilika.
Oscar Pistorius azidiwa na hisia mahakamani
Kwa Mujibu wa SAPA, hati za kortini zilizoandikishwa mwaka jana wakati mwanariadha huyo alipokuwa akiwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana zaonyesha kuwa nyumba hiyo iliyo katika mtaa wa Silverwoods ina thamani ya Randi millioni 5 ambazo ni sawia na dola za marekani 457 000.
Oscar anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake mnamo tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka jana huku akisema kuwa alimpiga risasi kimakosa.
Kesi ya mauaji dhidi yake ambayo kwa sasa iko katika wiki ya tatu, imehairishwa hadi siku ya jumatatu ambapo mashahidi wengine watano wa upande wa mashitaka wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kabla ya yeye kupewa fursa ya kujitetea.
Upande wa mashitaka unadai kuwa Pistorious alimpiga risasi Bi Steenkamp, aliyekuwa mwana mitindo, mtangazaji maarufu wa runinga na mwana sheria baada ya kinachodahniwa kuwa ugomvi wa nyumbani.
Huku kwa upande wake, Pistorious akisema kuwa aliamini kuwa mpenzi wake alikuwa amelala na akidhani kuwa palikuwa na mwizi nyumbani kwake alifyatua risasi kuelekea chooni asubuhi mapema mnamo tarehe 14 februari mwaka 2013.
Iwapo mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 27 atapatikana na hatia , huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha.
                                          source;bbc news
                                          The king star!

YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO IJUMAA.

DSC 0067 3583a
DSC 0068 eaacf
DSC 0069 5c13a
DSC 0070 c5ced
DSC 0071 f5ad3
DSC 0072 4b964
DSC 0073 3190f
DSC 0074 6785e
DSC 0075 87f9b
DSC 0076 fa0ed
DSC 0077 4c50c
DSC 0078 91a2a

Thursday, March 20, 2014

KWA MECHI HIZI ZILIZOBAKI NANI ATAWEZA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU MSIMU HUU KATI YA HIZI CLUB NNE?



MBEYA City Council FC

KINYANG`ANYIRO cha ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014, bado kinabaki kuwa kitendawili kwa timu zilizopo juu katika msimamo.

Sare ya bao 1-1 jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya vinara Azam fc dhidi ya Yanga imezidi kuweka mazingira magumu kwa mabingwa watetezi, Young African.

Katika mchezo huo  uliovuta hisia za mashabiki, Yanga walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Didier Kavumbagu, lakini Azam fc walisawazisha dakika za lala salama kupitia kwa kinda, Kevin Friday.

Hiyo ilikuwa mechi ya 19 kwa Yanga, wakati kwa Azam fc ilikuwa ya  20, huku wakijikusanyia pointi 44, wakati Wanajangwani wakivuna pointi 40 katika nafasi ya pili.

Yanga SC wamebakiza mechi 7, wakati Azam fc wamebakiza mitanange  6.

Wikiendi hii timu zote zitashuka dimbani. Yanga watasafiri mpaka mkoani Tabora kuwafuata maafande wa Rhino Rangers, wakati jumapili machi 23, Azam fc watawakaribisha JKT Oljoro,  uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Rhino Rangers ndio wanaoburuza mkia katika msimamo wakiwa wameshacheza mechi 21 na kujikusanyia pointi 13 tu kibindoni.

Kwa asilimia kubwa, maafande hawa wa Tabora, wameshachungulia kushuka daraja na inawezekana hakuna muujiza wa kubaki ligi kuu msimu huu kwasababu ya mazingira yao.

Mchezo dhidi ya Yanga utakuwa mkali endapo bado Rhino wanahitaji ushindi.

Lakini imani yao imeshuka na wanacheza bora liende na wameshapoteza matumanini ya kuendelea kucheza ligi kuu.

Pointi 13 kwa mechi 21 ni chache sana, zinahitajika nguvu za ziada kushinda mechi zote 5 walizobakiza, hapo sasa tunaweza kuzungumza mengine.

Yanga wataingia uwanjani wakiwa ma matokeo ya sare ya jana na suluhu ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita uwanja wa Jamhuri.

Yanga sc hawajafanya vizuri mechi zao mbili tangu watolewe na Al Ahly ligi ya mabingwa kwa penati 4-3, machi 9 mwaka huu, jijini Alexndria,  hivyo hawana cha kuwaza zaidi ya ushindi.

Kama watashindwa kupata ushindi katika mchezo huo, watakuwa wanazidi kuweka rehani ubingwa wao msimu huu.

Kwa maana hiyo, kocha mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm lazima awaeleze vijana wake umuhimu wa mechi ya jumamosi endapo wanahitaji ketetea taji lao.

Wakati Yanga wakiwa kwenye mawazo mazito juu ya mchezo huo, wapinzani wao, Azam fc watakuwa wanasubiria matokeo ili kujipanga kwa mchezo wa kesho yake.

JKT Oljoro  waliopoteza matumanini ya kusalia ligi kuu msimu , wataingia kuwavaa Azam fc ambao hawajapoteza mchezo mpaka sasa kwa lengo la kutafuta pointi tatu.

Mechi za karibuni zinaonesha kuwa Azam fc wamekuwa bora zaidi katika uwanja wao kwasababu  wanagawa dozi kubwa kwa wapinzani.

Mechi iliyopita waliwafunga Coastal Union mabao 4-0, hivyo JKT Oljoro wasipokuwa makini watachezea kipigo.

Endapo Azam fc watashinda mechi hiyo, watazidi kujikita zaidi kileleni, nao Yanga wakishinda watandelea kuwa wa pili.

Matokeo ya sare au suluhu hayatakuwa mazuri kwa Yanga, kwasababu Mbeya City waliopo nafasi ya tatu nao watacheza na JKT Ruvu jumamosi uwanja wa Chamazi.

Kama Yanga hawatashinda na Mbeya City wakapata matokeo ya ushindi, basi Yanga watashuka nafasi ya tatu.

Hata kama watatoa sare au suluhu mjini Tabora, bado Yanga watabaki nafasi ya tatu, kwani Mbeya City watakuwa wamefikisha pointi 42, Yanga 41.

Kama Yanga watashinda na Mbeya City watashinda, basi nafasi za pili na tatu zitabaki kama zilivyo.

Matokeo yoyote ya Yanga na Mbeya City hayatakuwa na athari kwa Azam fc katika nafasi ya kwanza, isipokuwa watasogelewa kwa pointi.

Wakati Yanga na Azam fc wakichunao vikali kusaka ubingwa, mechi zilizosalia kwa timu zote ni kama zifuatazo;

Yanga wamebakiza mechi dhidi ya Rhino Rangers itakayochezwa machi 22 mwaka huu uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Baada ya hapo atakuwa na mechi dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Taifa.

Ugumu wa mechi hizi mbili unatokana na mazingira ya Prisons na Rhino kwa sasa.
Hawataki kushuka daraja, zaidi Prisons wamedhamiria kubakia lihi kuu kuliko Rhino wanaoonekana kukata tamaa.

Haitakuwa kazi nyepesi kwa Yanga kuwafunga wajelajela hao uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.

Mechi nyingine zilizosalia kwa Yanga ni dhidi ya Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Hii pia itakuwa na changamoto kubwa kwasababu Mgambo wanajinusuru kushuka daraja msimu huu.

Pia Yanga wamebakiza  mechi dhidi ya Kager Sugar, Uwanja wa Taifa, mechi dhidi ya JKT Oljoro, jijini Arusha, mechi na JKT Ruvu uwanja wa Taifa.

April 19 mwaka huu Yanga watafunga msimu kwa kuvaana na Simba sc uwanja wa Taifa.

Katika mechi saba zilizosalia kwa Yanga, mechi mbili pekee ndizo atakutana na timu zilizopo salama msimu huu na zinahitaji nafasi nne za juu.

Kagera Sugar mpaka sasa wana uhakika wa kusalia ligi kuu pamoja na Simba sc ambao wanasaka nafasi za juu.

Mechi nyingine zote, Yanga atakutana na timu zinazopambana kukwepa mkasi wa kushuka daraja. Hivyo lazima ajiandae kwa nguvu zote kwasababu kukamiana kutakuwepo.

Kila timu inahitaji kupata ushindi bila kujali inakutana na timu kubwa au ndogo.

Kocha wa Yanga , Mholanzi, Hans Van Der Pluijm akisaidiwa na Charles Mkwasa wanahitaji  kutuliza sana akili zao kuelekea mechi hizo.

Azam fc amebakiza mechi sita ambazo ni dhidi ya JKT Oljoro, Mgambo, Ruvu shooting, JKT Ruvu, Mbeya City na Simba sc.

Mechi dhidi yaMbeya City itakayopigwa sokoine Mbeya, itakuwa ngumu zaidi kwa Azam fc kulingana na rekodi ya Mbeya City katika uwanja wake.

Mbeya City hawajawahi kufungwa kwao, hivyo lazima Azam fc wajiandae kama wanataka kuvunja rekodi hii.

Pia Mbeya City wanasaka ubingwa wa kwanza kama ilivyo kwa Azam fc. Tofauti ni umri katika ligi. Azam fc waliingia 2008/2009, Mbeya City waliingia 2013/2014.

Azam fc ameshakuwa makamu bingwa kwa zaidi ya misimu miwili, wakati Mbeya City ndio kwanza wanaanza kutafuta mafanikio.

Mechi hii itakuwa ngumu kwa timu zote mbili, matokeo yatategemea jinsi makocha wote wawili, Juma Mwambusi wa Mbeya City na Mcameroon, Joseph Marius  Omog wa Azam fc wamejipangaje.

Pia mechi dhidi ya Simba sc itakuwa mlima mwingine kwa Azam fc kwasababu Simba hawatakuwa na chakupoteza zaidi ya kusaka ushindi.

Kwa mazingira ya mechi za Azam fc, itakuwa ngumu kwake kupata ushindi kwenye baadhi ya mechi kwasababu wapinzani wake wanahitaji kujiweka vizuri katika msimamo.

Simba na Mbeya City wanawania nafasi za juu. Ruvu Shhoting anatafuta nafasi nzuri pia.

Mgambo, JKT Ruvu, JKT Oljoro wapo katika hatihati ya kukwepa kushuka daraja, hivyo mechi zao zitakuwa ngumu zaidi kutokana na kukutana na timu ambayo inaongoza ligi.

Haitakuwa kazi nyepesi kwa Azam fc kuibuka na ushindi katika mechi hizi, lakini kama watajiandaa vizuri basi wataweza kuvuna ushindi na kujihakikishia kutwaa ubingwa msimu huu.

Ligi ya mwaka huu imekuwa na changamoto kubwa kutokana na timu kubwa za Simba na Yaga kushindwa kufua dafu kwa Azam fc na Mbeya City.

Misimu ya nyuma, mpaka sasa ilikuwa rahisi kubashiri bingwa, na wakati mwingine timu ilikuwa inatangaza ubingwa kabla ya mechi tatu au nne.

Kwa msimu huu jambo hilo limebaki kuwa ndoto, ubingwa utaonekana mechi za mwisho, kwani mpaka sasa mbio bado zipo wazi kwa klabu zaidi ya moja.

Katika soka, hii ni hatua nzuri kwasababu inadhirisha zimekuweo timu zaidi ya mbili zenye ubora wa juu, tofauti na miaka ya nyuma iliyokuwa na ufalme wa Simba na Yanga.

Tuzidi kusubiri ili kuona nani ataibuka kidume katika nafasi nne za juu