Wednesday, October 8, 2014
RAISI KIKWETE KUKABIDHIWA KATIBA MPYA LEO.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania hii
leo anataraji kukabidhiwa katiba rasmi
iliyopendekezwa mjini Dodoma.
Tukio hilo la kihistoria linahitimisha
mchakato wa kikao cha Bunge maalum
la Katiba kilichomalizika mwishoni
mwa wiki iliyopita kwa kuipitisha
katiba tarajiwa kwa zaidi ya theluthi
mbili ambapo kwa sasa inasubiri
kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya
kupigiwa kura ya maoni hapo
mwakani.
Huku katiba hiyo mpya
iliyopendekezwa ikitarajiwa
kuwasilishwa kwa rais baadaye hii
leo, suala la kutojumuishwa moja kwa
moja kwa mahakama ya kadhi katika
katiba hiyo linaendelea kuwakera
baadhi pamoja na serikali kuahidi
kuliwasilisha bungeni kwa majadiliano
zaidi hapo baadaye.
bbc swahili..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment